Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Friday, August 16, 2013

Warioba afafanua Utanganyika


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,  Jaji Mstaafu Joseph Warioba, ametaka wenye ndoto ya kuwa na Katiba ya Tanganyika, kusubiri hadi muundo wa Serikali tatu utakapokubalika.
Jaji Warioba, alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma wakati akifungua baraza la  wawakilishi la  watu wenye ulemavu ambao wanaendelea kutoa maoni yao mjini hapa.
Alisema kuwa tume inayo mawazo ya Tanzania na ukiacha suala la Muungano, Zanzibar wamejikita zaidi kwenye muungano mengine yote yaliyo humu na migogoro mingine yanatoka Tanzania Bara.
“Wakitaka kutunga Katiba yao sijui kama watakuwa na maoni tofauti kuhusu haya, utakuta ni haya haya, kama wataongeza madiwani lakini hata hayo tayari yapo katika kumbukumbuku,” alisema Warioba.
Mjumbe huyo alisema iwapo wananchi wataamua kuwa na muundo wa serikali tatu wanaweza kutumia mawazo yaliyokusanywa wakati wa  mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Alisema tume yake inahifadhi kumbukumbu rasmi za maoni ya wananchi yote  ambapo  sura na sauti za Watanzania waliotoa maoni zimehifadhiwa ili kujua  wanachokitaka.
Kuhusu mfumo wa kukusanya maoni katika mabaraza ya Katiba ulioandaliwa na tume, alisema ni kuwagawa wananchi katika makundi kisha hugawiwa sehemu za rasimu kwa ajili ya kupitia kila kipengele, alikiri changamoto ambazo wanakabiliana nazo ni kuingiliwa kwa mchakato 

No comments:

Post a Comment