Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Monday, June 15, 2015

MBUNGE JOSEPH MBILINYI ALIPOHUDHURIA SHEREHE YA KIMILA YA WASAFWA

  • ILIHUSISHA MKUSANYIKO WA MACHIFU WOTE WA KABILA HILO
  • PICHANI CHIFU MKUU MWANSHINGA AKIMSIKILIZA MBUNGE


MBUNGE JOSEPH O. MBILINYI ANASOMESHA KUPITIA MFUKO WA ELIMU

( muendelezo wa SUGU NA ELIMU - 2 )..... 

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi "Sugu" anasomesha wanafunzi katika shule mbalimbali za sekondari, na hii ilitokana na baada ya kuanza kazi ya Ubunge moja ya changamoto aliyokumbana nayo ni wingi wa walezi na wanafunzi waliofika ofisini au waliomuona  kwa ajili ya kuomba msaada wa kusaidiwa ada na gharama nyingine za shule, ndipo ikapelekea aanzishe Mbeya Education Trust Fund (METF) au Taasisi ya Mfuko wa Elimu Mbeya.

Ambapo taasisi hii METF katika moja ya jukumu lake imeweza kusaidia wanafunzi wa sekondari  takribani 270 waliofaulu na hawakuwa na uwezo kutokana na  kuwa wanatoka kwenye familia zenye uwezo mdogo kiuchumi kwa kuwalipia ada na sare za shule pamoja na mahitaji mengine ya elimu pale inapobidi, na ilipoanza mwaka 2013 ilianza na watoto wa kidato cha 1 mpaka 4 (o'level) lakini sasa imeweza kusaidia mpaka wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 (A level).

Imetolewa na  OFISI YA MBUNGE MBEYA MJINI

(Chini ni picha mbalimbali za baadhi ya watoto wanaosomeshwa na Mfuko  huu wakiwa na Afisa wa METF)
Sunday, June 14, 2015

MBUNGE "SUGU" AIBUKIA KISIWANI MAFIA

• AFANIKIWA KUTOA VIONGOZI WA CHADEMA POLISI
• ATEMBELEA VIJIWE NA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA


Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA Joseph O. Mbilinyi "Sugu" wikiendi hii alikuwa kwenye ziara ya ujenzi wa Chama kwenye kisiwa cha Mafia na kufanikiwa kufanya mambo kadha wa kadha ya ujenzi wa Chama. 

Katika ziara yake hiyo ambayo licha ya kutembelea vijiwe mbalimbali na kubadilishana mawazo na wakazi wa kisiwa hicho pia alikumbana na mkasawa kushikiliwa kwa viongozi wa CHADEMA kisiwani hapo kwa makosa yasioeleweka ambapo kikosi hicho cha Mbunge huyo wa Mbeya waliweza kupigania mpaka usiku wa manane kuhakikisha viongozi hao wanatolewa polisi.

Pia katika ziara hiyo Mbunge pia aliweza kuongea na viongozi wa Kata katika jimbo hilo la Mafia pamoja na kusalimiana na vijana wa kikosi cha Red Brigade katika kisiwa hicho pamoja na kusaini kadi nyingi za CHADEMA ambazo wakazi wa kisiwa hicho walikuwa wakizihitaji kwa udi na uvumba. 

Baadaye jumapili aliweza kuongea na wakazi wa kisiwa hicho kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani hapo na kusisitiza elimu ya uraia ikiwemo kutoogopa vitisho vya polisi ambao ni vibaraka wa chama tawala.

Mbunge huyo pia alivutiwa na mandhari tulivu ya kisiwa hicho na huku akiwa amefikia katika chumba ambacho akina AC wala TV ambapo kwa madai yake alisema ni kizuri kwa utulivu na kutafakari.

KUTOKA OFISI YA MBUNGE MBEYA MJINI..... (SUGU NA ELIMU - 1)

IJUE PROGRAMU YA KOMPYUTA MASHULENI

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi anaendesha programu ya mafunzo ya kompyuta kwa wanafunzi wa sekondari za Kata zilizopo jijini Mbeya ambapo tayari ameanzisha madarasa ya kompyuta katika shule za sekondari tano (5)  kati ya 10 ambazo zitafikiwa na mradi huu kwa  awamu ya kwanza, shule hizo ni Shule ya Sekondari Mwakibete, Shule ya Sekondari Uyole, Shule ya Sekondari Forest, Shule ya Sekondari Iwambi na Shule ya Sekondari Iganzo. 

Lengo la programu hii ni kuhakikisha wanafunzi wa shule za Mbeya wanapomaliza kidato cha nne (4) wawe na uwezo wa kutumia kompyuta hali iliyopelekea kuongeza hadhi za shule na elimu kwa ujumla katika shule za Kata jijini Mbeya