Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Tuesday, November 22, 2011

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI AKA MR. SUGU AZUNGUMZIA KITABU CHAKE NA HARAKATI ZA KUINUA SANAA NCHINI

Mbunge wa Mbeya Mjini na Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kulia) Joseph Mbilinyi a.k.a Mr, SUGU akionyesha kitabu ambacho ameelezea maisha yake kitakachopatikana wakati wa Shoo ijulikanayo Anti Virus katika Tamasha la Burudani kwa washabiki2011 litaakalofanyika Nov. 26,2011 jijini Dar es Salaam lenye nia ya kuwapa fursa Wasanii wa hapa Nchini kujipatia Pesa na kunufaika na Sana hii ya Muziki wa Kizazi kipya, hali kadahlika Tamasha hili litahudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo, (kushoto) ni Msanii Fred Malaki a.k.a. MKOLONI.
 
Waziri kivuli wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Joseph Mbilinyi (a.k.a. MR. SUGU -alievalia kadeti) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana 21-nov-2011 kuhusu show ijulikanyo Anti Virus wakati wa Tamasha la Burudani kwa washabiki 2011-i litalaofanyika jijini DSM hapo Nov. 26 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi,(kushoto) ni Msanii Fred Malaki (a,k,a- MKOLONI) n a Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a ZAY –B, Katika tamasha hilo Wasanii mbalimbali watatumbuiza, -Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO,
Msanii Suma g akiimba mbele ya wana habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam jana.
 

Mheshimiwa Nchimbi mgeni rasmi uzinduzi wa Albamu ya Anti Virus 2
Gradice Sigera
Maelezo
Dar es Salaam
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Emanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya wanamuziki wa kizazi kipya inayoitwa Anti Virus 2.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam mratibu wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi alisema uzinduzi wa albamu hiyo unalengo la kuwakomboa vijana waweze kunufaika na kazi zao.
Mheshimiwa Mbilinyi amesema kwa muda mrefu wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakizulumiwa na wajanja wachache kitu ambacho kimewaacha wasanii hao kuendelea kuwa maskini.
"Kuna wajanja wachache ambao kwa muda wa miaka mingi wamekuwa wakinufaika na jasho la wasanii sasa tumeamua kufanya mapinduzi kwa kuwaungunisha wasanii ili waweze kutetea haki zao".Alisema Mheshimiwa Mbilinyi.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii tarehe 26 Novemba kuanzia saa 12-6 usiku ambapo jumla ya wasanii zaidi ya 20 watashiriki ikiwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge na mawaziri ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 5000.
Katika tamasha hilo Mheshimiwa Mbilinyi atauza kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake ambacho kitauzwa kwa shilingi 5000.
 
Asante kwa djSek,Gradice na Mwanakombo.!

Sunday, November 20, 2011

UJUMBE WA SUGU LEO

"naingia maelezo kwenye press,then naingia barabarani off to mbeya kesho ni siku yangu ya mahakama...jumatano narudi dar kumalizia promo ya concert ya nov 26 kwa kadri ya ratiba nitakayopangiwa na vinega...its kind'a hard being SUGU!!!"
Kwa kukumbusha tu Kesi ya Mh. Joseph Mbilinyi inasomwa tena Kesho tarehe 22-11-2011 Mahakama ya Mkoa iliyopo kwenye Jengo la Mahakama Kuu maeneo ya Forest Mbeya,
Mr. II Sugu  atapandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ambayo anatuhumiwa kufanya kusanyiko la umma kinyume cha sheria.


Saturday, November 12, 2011

Mh SUGU ATEKA MBEYA,, VURUGU KWISHA!!! MACHINGA HURU KUFANYA BIASHARA KAMA MWANZO

Maelfu ya wakazi wa jiji la Mbeya  wakimsikiliza kwa makini Mbunge wao 

 
Mh SUGU akizungumza na umati wa wakazi  wa jimbo la Mbeya mjini ambao wakisubili tamko lake kwa hamu
Mh Diwani , kata ya Forest akimkaribisha Mh Sugu (  Gorofa la OTU eneo lililo tumika kama jukwa kutokana na umati mkubwa wa wanambeya )Maelfu waki msindikiza Mbunge wao ofisi ya CHADEMA wilaya


Jiji la zizizima kwa hoi hio  na ndelemo 
Mzungu nae hakuwa nyuma kuonyesha ishara inayotumiwa na  CHADEMA huku akisema Peoplessssssss......
umati ukiitikia  Powerrrrrrrrrrr !!!!!!!!!!!!!!!!!!


Umati uli sikuma gari laMbunge  kwa takribani kilomita mbili kutoka Kabwe hadi Ofisi ya chama wilaya.
Hapa  Mh Sugu akiwashukuru wananchi kwa kumsindikiza hadi ofisi za Chama cha CHADEMA  eneo la Mama John.


Wananchi wakirudi nyumbani baada ya kumsindikiza ofisini mbunge ya Mh Joseph Mbiliyi
Baada ya mkutano Mh  Sugu alikwenda moja kwa moja Hospitali ya RufaaMbeya kuwaona majeruhi wa vuruguza Machinga na Polise


Mh Joseph Mbilinyi akiingia wodi namba 1 ya Hospitali ya Rufaa Mbeya kuwataka hali majeruhi wa vurugu za Machinga na police 


na haya ni baadhi ya majina ya walio jeruhiwa na kulazwa katika hodi namba 1 hapa hospitali ya Rufaa

VURUGU JIJINI MBEYA JANA NA LEO

Risasi za moto zimetumika pia


Mwandishi wa Tanzania Daima na ITV wakifuta machozi baada ya kupigwa bomu !!!!!!!!!!!
Kamata kamata iki endelea mitaa ya Kabwe

Friday, November 11, 2011

MAPAMBANO BADO YANAENDELEA KATI YA POLISI NA WAMACHINGA JIJINI MBEYA

 

Baadhi ya wamachinga wakiwa wamelipindua gari yaina ya toyota na kusimama juu yake huku wakitamka maneno makali kwa polisi na jiji la mbeya kwa kuwanyanyasa katika biashara zao
Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao
Wamachinga wakiwazomea polisi eneo la kabwe
Maduka yote eneo la mwanjelwa mpaka uyole yamefungwa
Moja ya gari lililobinuliwa na kuwekwa katikati ya barabara ya mbeya tunduma
Huu ndiyo mtaa wengi huuita mtaa wa kasisi uliyosababisha vurugu zote kati ya wamachinga na askari wa jiji  
Mmachinga akiwarushia jiwe kwa kutumia manati yaani ni hatari tupu
Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana
Naye mwandishi wetu  wa mbeya yetu Joseph Mwaisango alionja joto ya jiwe baada ya kutupwa ndani ya gari ya polisi kwa kosa la kupiga picha matukio hayo ya wamachinga na polisi  baadaye aliachiwa na kuendelea na kazi yake
RISASI ZA MOTO NAZO ZIMETUMIKA KATIKA TUKUKIO HILI
MABOMU YA MACHOZI NDIYO USISEME KILA MAHALI YAMETAPAKAA
Mwenye kofia haya mwenye supu haya kila mmoja alikua anaokoa uhai wake
Hayo ndiyo maandishi yaliyoandikwa barabarani

kwa ufupi vurugu zinaendelea  zimefika uyole kati hali si shwali barabara zimefungwa sasa nizaidi ya masaa 10 hakuna usafiri yati mbeya iringa wala mbeya tunduma habari kamili tutawaketea baadaye
Asante Mbeya Inogile...