Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Friday, August 30, 2013

MA MISS MBEYA CHADEMA WALONGA


 Inaongeza kujiamini, kujua haki zako na kupunguza uzee  .... Ma Miss wazee wasema inasaidia kujisikia kijana.

Thursday, August 29, 2013

Chadema: Tutapeleka mapendekezo yetu Katiba mpya kwa lori

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefunga rasmi mikutano yake ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Rasimu ya Katiba mpya kupitia mabaraza huru ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.   Chama hicho kimesema kimefanikiwa kukusanya maoni ya wananchi milioni tano na kwamba wanatarajia kupeleka maoni hayo kwenye ofisi za Tume kwa lori kwa kuwa ni mengi. 
Akifunga mikutano hiyo juzi jijini humo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alisema katika mikutano 49 waliyoifanya ndani ya mikoa tisa nchini, wamekusanya takribani maoni milioni tano kutoka kwa Watanzania kuhusu maboresho ya rasimu hiyo dhidi ya milioni mbili yaliyokusanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa wanachama wake.


Dk. Slaa alitoa kauli hiyo juzi katika viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, wakati akihitimisha mkutano wake wa mabaraza huru ya kukusanya maoni kwa Watanzania juu ya Rasimu ya Katiba mpya. Alisema, Chadema wanaunga mkono  Rasimu ya Tume ya  Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, lakini wanapingana naye katika baadhi ya vipengele kama vile Tanzania Bara kuitwa Tanganyika.


Baadhi ya wananchi waliokuwapo kwenye mkutano huo walipendekeza kuongezwa kwa vipengele vya haki kwenye tunu za taifa.Tunu saba za taifa ambazo zimependekezwa katika rasimu hiyo ni utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya taifa.


Wananchi hao walipendekeza kwamba kwenye rasimu hiyo kiongezwe kipengele kinachomruhusu kila Mtanzania kuwa na haki ya kumiliki ardhi, kupata huduma bora za afya kama viongozi wa serikali na wabunge wanavyofanyiwa.


Dk. Slaa alisema katika mikutano hiyo  wamezunguka katika mikoa tisa na kufanya mikutano 49 huku zaidi ya Watanzania milioni tano wakiwa wametoa maoni yao juu ya rasimu hiyo.

Tuesday, August 27, 2013

SUGU: AWAAMBIA BODABODA “ Wakijipendekeza….vuteni kisha mnawabwaga”

Kufuatia lindi la Wanasiasa ambao wanapita huku na huko kwa ajili ya kuonga vitu mbalimbali ovyo na kusingizia ni misaada, Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi amewaambia madereva wa pikipiki za biashara almaarufu kwa jina la bodaboda kuwa kama wanasiasa wakija kuwaonga walambe mshiko lakini wazidi kuwabwaga linapokuja sanduku la kura kama ilivyotokea juzijuzi kwenye uchaguzi wa Udiwani  kata ya Iyela Mbeya mjini ambapo fedha zilimwagwa kwa wingi haswa kwa makundi ya vijana ikiwemo madereva wa bodaboda lakini CHADEMA kikashinda kwa kishindo.

Sugu amesisitiza kuwa, kama wangekuwa wanapenda maendeleo yenu basi wangetekeleza sera mbalimbali za kuwakomboa vijana, ambazo kwenye makaratasi yao wameandika tena kiumahiri ikiwemo mipango yao ya ajira walioahidi lakini hakuna utekelezaji...zaidi zaidi ni ubadhirifu wa fedha kila kukicha ambazo wangekuwa na mapenzi ya dhati ya kuwasaidia ingekuwa wamewasaidia vijana kwa kiasi kikubwa, mfano hela wanazolipwa Dowans ni nyingi sana na mzigo kwa Mtanzania na mbaya zaidi kinachouma  mpaka sasa hakuna mtu ambaye yuko jela kutokana na  uzembe huo uliofanyika”Friday, August 23, 2013

MH. JOSEPH MBILINYI ADHIIRISHA YEYE BADO NI SUGU....

 Wananchi wa Mbeya wakilipuka kwa furaha baada ya kumwona Mbunge wao Joseph Mbilinyi...

 Mh. Joseph Mbilinyi akiwa amekaa meza kuu na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe
 Sugu akisimama kwenda kuongea na wana Mbeya jukwaaani..
 aka. "Rais wa Mbeya" akiongea huku wananchi wake wakimsikiliza kwa makini...
 Nyomi lililokuwemo uwanjami hapo wakifurahia jambo kutoka kwa Joseph Mbilinyi..


 Wana Mbeya wakilipuka kwa furaha pale Mbunge wao alipowakebehi wapinzani wake kwamba CHADEMA haing'ooki Mbeya 2015 zaidi zaidi ni lazima wachukue Hlmashauri...

 Mbunge wa Mbeya Mjini akiongea na wananchi wa Mbeya...


 Sugu akimalizia kuongea na Wananchi wa Mbeya na kugeuka nyuma kumkaribisha kiongozi mwingine...

Hapa Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimkaribisha Mh. Mbunge Silinde "Sauti ya Simba" aungurume jukwani..

MBWEMBWE ZA CHOPA YA CHADEMA ZAWAPAGAWISHA WANA-MBEYA: TAZAMA HATUA KWA HATUA...Ilikuwa kama sinema

 Mwanzo ilionekana kwa juu sana ikipita kwenye anga la Mbeya...

Ikarudi ikipita huku ikiwa imesogea zaidi...


 Wananchi wa Mbeya wakiitazama wakati inaanza kutua....
 Chopa hapo inaongozwa kutua...
 Chopa ikikaribia ardhi...
 Hapo ikiwa tayari imetua ardhini...
 

 Hapo imeanza kuonekana vizuri...
 Mbunge Joseph Mbilinyi akiwa na viongozi wa CHADEMA Mbeya tayari kupokea wageni..


 Rubani akifungua mlango wa Mwenyekii wa CHADEMA Freeman Mbowe....

 Viongozi wa CHADEMA Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mbunge Tundu Lisu na Mbunge Silinde wakishuka...

 Hapo Mwenyekiti na Viongozi wengine wa Chama wakianza kuelekea Jukwaani..
 

 Ilikuwa tabu kwa Mwenyekiti na viongozi wengine kuelekea jukwaani watu walijaa wakitaka kushikana mkono na viongozi....


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akijiandaa kukaa jukwaani

 Wananchi wa Mbeya wakiwa makini kusikiliza hotuba mbalimbali za viongozi huku Chopa ikionekana kwa mbali...
 Baadaye Mwenyekiti Freeman Mbowe akakaribishwa na Tundu Lisu jukwaani...
 Wananchi wakishangilia baada ya Mwenyekiti kabla ya kuhutubia, kutangaza kuwa ameamua kulala Mbeya na ataondoka kwa maandamano hivyo Chopa iondoke.. Watu wakigeuka nyuma kuiangalia Chopa inavyoanza kunyanyuka...
 Chopa ikiwa imeganda hewani tayari kwa kuondoka...
Chopa ikipita karibu na jukwaa huku Mwenyekiti na wananchi wakiitazama inaondoka...

 Ghafla ilirudi kwa mbwembwe na kufanya Mwenyekiti kuacha kuhutubia na kuitazama inavyoishia..

 Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akicheka bada ya Chopa kuishia kwa mbwembwe eneo la mkutano...
 Mh. Freeman Mbowe akaendelea kuongea na wananchi wa Mbeya kuhusu umuhimu wa kushiriki kwao katika zoezi la utengenezaji katiba mpya...