Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Tuesday, August 27, 2013

SUGU: AWAAMBIA BODABODA “ Wakijipendekeza….vuteni kisha mnawabwaga”

Kufuatia lindi la Wanasiasa ambao wanapita huku na huko kwa ajili ya kuonga vitu mbalimbali ovyo na kusingizia ni misaada, Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi amewaambia madereva wa pikipiki za biashara almaarufu kwa jina la bodaboda kuwa kama wanasiasa wakija kuwaonga walambe mshiko lakini wazidi kuwabwaga linapokuja sanduku la kura kama ilivyotokea juzijuzi kwenye uchaguzi wa Udiwani  kata ya Iyela Mbeya mjini ambapo fedha zilimwagwa kwa wingi haswa kwa makundi ya vijana ikiwemo madereva wa bodaboda lakini CHADEMA kikashinda kwa kishindo.

Sugu amesisitiza kuwa, kama wangekuwa wanapenda maendeleo yenu basi wangetekeleza sera mbalimbali za kuwakomboa vijana, ambazo kwenye makaratasi yao wameandika tena kiumahiri ikiwemo mipango yao ya ajira walioahidi lakini hakuna utekelezaji...zaidi zaidi ni ubadhirifu wa fedha kila kukicha ambazo wangekuwa na mapenzi ya dhati ya kuwasaidia ingekuwa wamewasaidia vijana kwa kiasi kikubwa, mfano hela wanazolipwa Dowans ni nyingi sana na mzigo kwa Mtanzania na mbaya zaidi kinachouma  mpaka sasa hakuna mtu ambaye yuko jela kutokana na  uzembe huo uliofanyika”No comments:

Post a Comment