Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, July 26, 2014

Thursday, July 24, 2014

VIONGOZI CCM WATIMULIWA MKUTANONIKushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM, Mkoani Mbeya, Fatuma Kasenga (aliyekumbwa na dhahama hiyo), akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilayani Rungwe, Mwalimu Peter Gwandege Nkanje.
Wananchi wa Kata ya Kambasegela wilayani Rungwe mkoani hapa, wamewafukuza viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wa kata hiyo walipotaka kufanya mkutano wa hadhara ili kuimarisha chama chao.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga, Katibu wa jumuiya hiyo Kata ya Kambasegela, Frank Mwansasu, alisema wananchi walimtimua yeye na msafara wake kwa madai kwamba waliahidiwa maji zaidi ya miaka kumi sasa bila kupatiwa.
“Mwenyekiti, kero yangu kubwa ni kwamba, mimi na wenzangu tulifukuzwa na wananchi tusifanye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yetu ya kata, wananchi wanasema waliahidiwa maji, lakini hawajapelekewa mpaka hivi sasa,” alisema Mwansasu.
Akijibu kero hiyo, Mwenyekiti Kasenga, alisema hayo ni matokeo ya baadhi ya viongozi kutowajibika vema katika nafasi zao.
Alisema suala hilo limemsikitisha, na kwamba yeye na msafara wake watalifikisha kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi, ili kulipatia ufumbuzi.
Akiwa katika ziara hiyo, mwenyekiti huyo alipokea kero nyingine kwa baadhi ya wananchi wa Kata ya Nkunga, ambao walimwambia kuwa chama hicho kinachukiwa kwa udhaifu wa baadhi ya viongozi wake.
Wananchi walisema kata hiyo ina uhitaji wa umeme, na kwamba katika Kijiji cha Ibililo, kuna msigano wa viongozi, jambo ambalo linasababisha kutopatikana kwa maendeleo ya kijiji.
“Jitokezeni kwenye marekebisho ya daftari la kudumu la mpiga kura na ukifika wakati wa uchaguzi, wazee, vijana na wanawake wanaofaa wapeni nafasi wagombee,” alisema Kasenga.
  • Gordon Kalulunga
· 

TASWIRA: MBUNGE JOSEPH MBILINYI "SUGU" ALIPOONGEA NA WAKAZI WA MAENDELEO/SOKOMATOLA JIJINI MBEYA


Saturday, July 19, 2014

JOSEPH MBILINYI "SUGU" AITEKA MAFINGA, MUFINDI - IRINGA.

  • NI KATIKA MUENDELEZO WA OPERESHENI KOMBOA MUFINDI
  • OFISI ZA CHADEMA KATA KUANZA KUJENGWA MUFINDI YOTE
  • WILLY MUNGAI “BIG WILLY” AKABIDHI HUNDI NA KUELEZEA  MPANGO HUO
  • PATRICK OLE SOSOPI NA MWAMBIGIJA “MZEE WA UPAKO" WATOA MISUKULE
                      
 Mgeni Rasmi Mbunge Joseph Mbilinyi wa Mbeya akipokea hundi ya Tsh. 2,500,000 kutoka kwa William Mungai "Big Willy" katika kikao cha uzinduzi wa programu maalumu ya ujenzi wa ofisi za CHADEMA katika kata zote za Mufindi Kusini.
  
William Mungai "Big Willy" akielezea kwa kina jinsi ambavyo program ya kujenga ofisi za CHADEMA katika kata zote za Mufindi Kusini utakavyotekelezwa.
 
             Mgeni Rasmi Mbunge wa Mbeya Mjini akiongea na wana Mufindi katika kikao hicho

 Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Mwambigija "Mzee wa Upako" akisisitiza jambo katika kikao hicho.

 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiongea na wana Mufindi katika Kikao ambacho kiliambatana na uzinduzi wa Programu ya Ujenzi wa Ofisi za Kata Mufindi.
 
 Makamanda wakiwa wanajadiliana kabla ya kuelekea kwenye Mkutano wa Hadhara
 
 Mh. Joseph Mbilinyi akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Bw. Mwambigija wakiingia eneo la mkutano wa hadhara Mafinga.
 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Sera, Itikadi na Utafiti wa CHADEMA Kanda za Nyanda za Juu Kusini akiwakilisha Mkoa wa Iringa Bw. Patrick Ole Sosopi akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.

 Kamanda William Mungai "Big Willy" akifafanua changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa hususani wana Mufindi.
 
 Umati wa wana Mafinga - Mufindi ukiwa umejaa katika Uwanja wa mashujaa ambao aukutosha na kusababisha watu wengine wasikilizie hotuba mbalimbali wakiwa nje ya Uwanja.

Makamanda wakiwa wamekaa  meza kuu huku wakifuatilia mkutano huo wa hadhara.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Kamanda John Mwambigija almaarufu kama "Mzee wa Upako" akiwa jukwaani kutoa misukule ya CCM.
 
 Mbunge Joseph Mbilinyi "Sugu" akijiandaa kupanda jukwaani huku akipunga mikono wakati wimbo wake maarufu "WANAKUITA SUGU..." ukiwa unasikika.....

 Joseph Mbilinyi "Rais wa Mbeya" akiwa makini kuangalia umati wa watu uliofurika mara baada ya kupanda jukwaani.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini akiwa jukwaani kuongea na wana Mafinga kuhusu changamoto mbalimbali  zinazowakabili Tanzania pamoja na  mustakabali wa zoezi la Katiba mpya jinsi ambavyo linavyochakachuliwa.
 
 Umati wa wana Mafinga uliofurika ndani na nje ya uwanja wa Mashujaa ukimsikiliza Mbunge huyo.

 Wazee wakimpongeza Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya kushuka jukwaani.
 
Kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge Joseph Mbilinyi Ndg. Kwame Elly Anangisye , Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini John Mwambigija "Mzee wa Upako", Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi " Sugu" na Kamanda Patrick Ole Sosopi wakisimama tayari kwa kuondoka mara baada ya mkutano.


Wednesday, July 16, 2014

MBUNGE JOSEPH MBILINYI "SUGU" AFANYA ZIARA MTAA WA TONYA - ITUHA, JIMBONI MBEYA MJINI

  •  APATA FURSA YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUONGEA NA WAKAZI WA ENEO HILO
  • VIJANA WALIOCHUKUA KADI ZA CCM SIKU CHACHE ZILIZOPITA WAZISALIMISHA
  • WADAI WALIKUWA NA SHIDA NA SHILINGI 5,000 ZILIZOKUWA ZIKIGAWIWA
 Vijana wa Mtaa wa Tonya - Ituha walimpokea Mbunge wao kuelekea Tonya


 Msafara wa Mbunge kuelekea Mtaa wa Tonya

Mbunge alilakiwa na kikundi cha ngoma cha vijana
 
Mbunge Joseph Mbilinyi akicheza ngoma baada ya kuwasili mtaa wa Tonya

 Msafara wa Mbunge ukaelekea kufungua Ofisi ya CHADEMA -Tonya

Mh. Joseph Mbilinyi akiongea kabla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Tonya ambaye naye ameshiriki katika kuikamilisha

Hapa Mbunge Sugu akijiandaa kuzindua ofisi

 Akisaini kitabu cha wageni kuonyesha kuwa ofisi imefunguliwa rasmi
 
 Baada ya zoezi hilo Mbunge alipelekwa na diwani kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa daraja katika mtaa wa Tonya

 Hapo Mbunge Joseph Mbiliyi akiongea na wakazi wanaoishi kandokando ya daraja hilo

 Pia Mbunge alipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari ambapo madarasa mapya yamejengwa


Joseph Mbilinyi "Sugu" hapo akiwa katika mkutano wa hadhara katika Mtaa huo wa Tonya

 Wazee nao walikuwepo kusikiliza Mbunge akielezea shuhuli za kimaendeleo zilizofanyika jimboni

 Mmoja wa Kijana maarufu wa eneo hilo ambaye alichukua kadi ya CCM siku chache zilizopita alirudisha kadi  kwa Mbunge na kuelezea kuwa alichukua  kwa  kuwa alikuwa akihitaji shilingi 5,000 zilizokuwa zinagawiwa na CCM kwa vijana ili wagawiwe kadi hizo za CCM

 Kijana  mmojawapo wa aliyechukua kadi ya CCM siku chache zilizopita akinyanyua kadi ya CHADEMA aliyokabidhiwa na Mbunge

 Wazee wakimshukuru Mbunge kwa kuwa mwakilishi wao mwema katika jimbo la Mbeya mjini

 Vijana wakikabidhiwa kadi za CHADEMA na mbunge wao


 Vijana wakiwemo ambao walirudisha kadi za CCM siku chache zilizopita wakiwa wanaonyesha kadi zao za CHADEMA walizokabidhiwa na Mbunge

 Wananchi wakionge na Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya mkutano wa hadhara Baadaye Mbunge Sugu alimalizia na kikao cha ndani na baadhi ya wakazi wa Tonya ambapo pia alipata fursa ya kupokea maoni na maswali na pia alitolea ufafanuzi mambo mbalimbali