Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, July 12, 2014

MBUNGE SUGU: AKABIDHI KAZI YA UJENZI WA DARAJA LA IYELA(MAKABURINI)

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" amekabidhi kazi ya ujenzi wa daraja la Iyela(makaburini) kwa mkandarasi na tayari ujenzi huo umekwisha anza, daraja hilo kwa mujibu ya maelezo litajengwa likiwa limenyanyuliwa sana juu na litakuwa likipitisha magari yenye uzito hadi  tani 10, na  pichani ni kivuko ambacho kilianza kujengwa miaka zaidi ya 25 iliyopita na hakikukamilika.
Kwa wakazi wa Mbeya daraja hilo ni muhimu sababu ndiyo wanaitumia wananchi wa Mbeya kwa shughuli zao mbalimbali na haswa maziko sababu ndiyo eneo lina makaburi yanayotumiwa sana na wakazi wa Mbeya kwa maziko, na tatizo la daraja hilo lilipelekea watu kuzunguka umbali mrefu ili kufikia eneo hilo.

 

No comments:

Post a Comment