Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Wednesday, July 9, 2014

WAANDAMANA KUDAI KIDATO CHA TANO

  • WATINGA OFISI ZA MBUNGE JOSEPH MBILINYI NA MKUU WA MKOA 
  • WAANDISHI WA HABARI NAO WATINGA KUJUA HATIMA YA SAKATA HILI 
  • SUGU AONGEA NA WAZIRI NA KUHAKIKISHIWA SUALA HILI  LITATATULIWA MAPEMA
  • Wahitimu 39 wa kidato cha nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana waliandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa na pia wakaenda kwa Mbunge wa Mbeya Mjini ili kujua hatma yao baada Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kuwapangia nafasi za kujiunga kidato cha tano licha ya kufanya vizuri katika mitihani yao.
    Wakizungumza wanafunzi na wazazi wao, walisema kuwa waliamua kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa  pamoja na Mbunge wa Joseph Mbilinyi - Sugu  ili kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi majibu ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wa chini yake.
     
    Walisema tangu wizara itangaze majina kwa ajili ya kujiunga kidato cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa kuona wanafunzi kutoka shule hiyo hawajapangiwa kwa ajili ya kuendelea na masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa na ufaulu mzuri.
    Wanafunzi hao ambao wamepata alama za daraja la kwanza hadi tatu, hawajui hatima yao kutokana na wizara husika kushindwa kuwapangia shule kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
    Nao wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa, hakuna majina ya watoto wao na hatima ya watoto wao kwa sasa iko chini ya Mbunge wao huyo ili awasaidie kutatua hili suala.
     
    Mbunge huyo wa Mbeya mjini aliweza kuongea na Naibu Waziri wa Tamisemi - Elimu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri huyo kumuhakikishia kuwa tatizo hilo lililotokana na Baraza la mitihani kutofikisha majina ya wanafunzi hao wizarani kwa wakati lakini limeshafika mezani kwake hivyo atahakikisha linatatatuliwa ndani ya siku chache zijazo.
    Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika shule hiyo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa ajili ya kuendelea na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa alama nzuri.


     
     

No comments:

Post a Comment