Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, July 19, 2014

JOSEPH MBILINYI "SUGU" AITEKA MAFINGA, MUFINDI - IRINGA.

  • NI KATIKA MUENDELEZO WA OPERESHENI KOMBOA MUFINDI
  • OFISI ZA CHADEMA KATA KUANZA KUJENGWA MUFINDI YOTE
  • WILLY MUNGAI “BIG WILLY” AKABIDHI HUNDI NA KUELEZEA  MPANGO HUO
  • PATRICK OLE SOSOPI NA MWAMBIGIJA “MZEE WA UPAKO" WATOA MISUKULE
                      
 Mgeni Rasmi Mbunge Joseph Mbilinyi wa Mbeya akipokea hundi ya Tsh. 2,500,000 kutoka kwa William Mungai "Big Willy" katika kikao cha uzinduzi wa programu maalumu ya ujenzi wa ofisi za CHADEMA katika kata zote za Mufindi Kusini.
  
William Mungai "Big Willy" akielezea kwa kina jinsi ambavyo program ya kujenga ofisi za CHADEMA katika kata zote za Mufindi Kusini utakavyotekelezwa.
 
             Mgeni Rasmi Mbunge wa Mbeya Mjini akiongea na wana Mufindi katika kikao hicho

 Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Mwambigija "Mzee wa Upako" akisisitiza jambo katika kikao hicho.

 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiongea na wana Mufindi katika Kikao ambacho kiliambatana na uzinduzi wa Programu ya Ujenzi wa Ofisi za Kata Mufindi.
 
 Makamanda wakiwa wanajadiliana kabla ya kuelekea kwenye Mkutano wa Hadhara
 
 Mh. Joseph Mbilinyi akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Bw. Mwambigija wakiingia eneo la mkutano wa hadhara Mafinga.
 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Sera, Itikadi na Utafiti wa CHADEMA Kanda za Nyanda za Juu Kusini akiwakilisha Mkoa wa Iringa Bw. Patrick Ole Sosopi akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.

 Kamanda William Mungai "Big Willy" akifafanua changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa hususani wana Mufindi.
 
 Umati wa wana Mafinga - Mufindi ukiwa umejaa katika Uwanja wa mashujaa ambao aukutosha na kusababisha watu wengine wasikilizie hotuba mbalimbali wakiwa nje ya Uwanja.

Makamanda wakiwa wamekaa  meza kuu huku wakifuatilia mkutano huo wa hadhara.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Kamanda John Mwambigija almaarufu kama "Mzee wa Upako" akiwa jukwaani kutoa misukule ya CCM.
 
 Mbunge Joseph Mbilinyi "Sugu" akijiandaa kupanda jukwaani huku akipunga mikono wakati wimbo wake maarufu "WANAKUITA SUGU..." ukiwa unasikika.....

 Joseph Mbilinyi "Rais wa Mbeya" akiwa makini kuangalia umati wa watu uliofurika mara baada ya kupanda jukwaani.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini akiwa jukwaani kuongea na wana Mafinga kuhusu changamoto mbalimbali  zinazowakabili Tanzania pamoja na  mustakabali wa zoezi la Katiba mpya jinsi ambavyo linavyochakachuliwa.
 
 Umati wa wana Mafinga uliofurika ndani na nje ya uwanja wa Mashujaa ukimsikiliza Mbunge huyo.

 Wazee wakimpongeza Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya kushuka jukwaani.
 
Kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge Joseph Mbilinyi Ndg. Kwame Elly Anangisye , Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini John Mwambigija "Mzee wa Upako", Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi " Sugu" na Kamanda Patrick Ole Sosopi wakisimama tayari kwa kuondoka mara baada ya mkutano.


No comments:

Post a Comment