Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Tuesday, August 31, 2010

SIKU WASANII WALIPOJITOSA RASMI NA HARAKATI CHAMANI

             

Wabunge Mbeya wazomewa mbele ya Kikwete

 MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete juzi aliendelea na mikutano yake ya kampeni katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya ambapo katika mikutano yake wagombea ubunge walizomewa.Kikwete aliwasili mkoani Mbeya jana na kuanzia kampeni zake kwenye mji mdogo wa Tunduma ambao uko mpakani mwa Zambia na ambao una pilikapilika nyingi za wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hiyo jirani.

Tofauti na mikutano mingine ya kampeni katika majimbo mbalimbali ambayo ameshatembelea kwenye kampeni zake, Kikwete alikumbana na hali isiyo ya kawaida wakati alipowanadi kwa nyakati tofauti wagombea hao wa majimbo ya Nkasi Kusini, Desderius Nipata na wa Mbozi Kusini, Lucas Siyame.
Tukio la kwanza la kuzomea lilitokea kwenye Uwanja wa Kate, ulio katika Kata ya Kate ambako wananchi walizomea baada ya mgombea wa Jimbo la Nkasi kuwataka wampigie kura KikweteLakini alipoanza kuomba wananchi hao wampigie kura na yeye ili afanye kazi na Kikwete, wananchi hao walianza kumzomea.

Mjini Mbozi tukio la mgombea ubunge kuzomewa lilimkumba Dk Lucas Siyame baada ya kuitwa jukwaani na Kikwete ili awasalimie wananchi baada ya kumaliza hotuba yake fupi kutokana na kuwa na mkutano mwingine kwenye mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi ambao, hata hivyo, uliahirishwa hadi leo asubuhi."Sipo peke yangu, jamani nawaombea kura pia madiwani, na mbunge,’ alisema Kikwete lakini kauli hiyo ilipokewa na kelele za wananchi waliokuwa wakipiga kelele kusema “maji, maji, maji, hatutamtaki huyo.”
Wananchi hao walipiga mayowe hayo huku wakionyesha ishara ya vidole viwili ambayo ni alama ya Chadema, hali iliyomaanisha kuwa wanamuunga mkono mgombea wa chama hicho cha upinzani.
Upepo wa kisiasa kwenye mji huo haujaikalia vizuri CCM kutokana na hali ilivyojionyesha dhahiri kwenye mkutano huo. Wakati baadhi ya watu walionekana kumkubali Kikwete, wengine walikuwa wakipiga miluzi na baadhi kuonyesha ishara ya vidole viwili.

Baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake, wananchi hao walipiga miruzi na kunyoosha mikono juu wakionyesha alama za vidole viwili kuashiria kuikubali Chadema.
Awali kulikuwa na dalili za wazi kumkubali Kikwete na kumpimnga Dk Siyame na wananchi wengi walitaka kuzungumza na wanahabari kueleza kero yao. Baadhi waliiambia Mwananchi kuwa wana shida kubwa ya maji pamoja na serikali kutoa zaidi ya Sh600 milioni kwa mradi wa maji, fedha walizodai zimeliwa huku mbunge huyo akikaa kimya.

Baadhi ya wananchi walisikika wakisema, kura zetu za ubunge tutampa wa upinzani. Huyu Siyame hajaonekana hapa tangu achaguliwe miaka mitano iliyopita,” alisema mmoja wa wakazi hao wa Mbozi.

Monday, August 30, 2010

MATUKIO YALIYOJIRI UZINDUZI CHADEMA KITAIFA - JANGWANI


                              maelfu ya wanachadema waliofika katika viwanja vya jangwani leo.


                                             Msanii G- Solo akishambulia jukwaa leo.

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiimba moja ya nyimbo zake ujulikanao kwa jina la ‘Sugu’ ambao ulionekana kuwachangamsha vijana wengi waliofika viwanjani hapo jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho pamoja na Ilani yake

                                   moja ya vioja vilivyokuwepo katika viwanja vya jangwani leo

Mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mkoloni ambaye pia ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma lisala fupi kwa niaba ya Wasanii wenzake kuhusiana na mambo mbali mbali yanayoikumba anga ya muziki na wanamuziki wenyewe,Mkoloni baadae lisala hiyo aliikabidhi kwa mgombea Urais wa chama hicho Dr.Willbroad Slaa.

Sunday, August 29, 2010

SUGU ALISIMAMISHA JIJI KWA MUDA

             Umati wa watu ukilisukuma gari alilopanda Joseph Mbilinyi (Mr II - Sugu).

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya na mwanaharakati Joseph Milinyi (Mr II - SUGU) ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Mbeya mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ameshangaza jiji baada ya lundo la watu kumsindikiza kwa kusukuma gari alilokuwemo baada ya kutoka jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni wa CHADEMA kitaifa.

SUGU ambaye alivuta hamasa ya watu wengi waliohudhuria uzinduzi huo alikuwa ni mmoja wa watu waliopanda jukwaani kuhamasisha na alitumia kipaji chake kutoa ujumbe kupitia baadhi ya nyimbo ambazo zilimchukulia umaarufu mkubwa alizotoa miaka ya nyuma.

Baada ya mkutano umati wa watu ulimzuia kuingia kwenye gari hadi alipoongea nao na kuwasihi wamruhusu kwenda sababu kuna kikao anawahi, baada ya kupanda gari hilo ambalo kulikuwa na wasanii wengine, Wanaharakati Mkoloni, G Solo na Dan Msimamo wananchi walianza kulisukuma huku wakipiga mayowe kumshangilia na huku wakiimba kwa vionjo  mbalimabali, ikiwemo kiitikio "Sugu, tumemuona Mbunge wa Mbeya" walilisukuma gari hilo mpaka walipoingia barabara ya Morogoro eneo la jangwani na kuzuia magari yote yaliyoyakitokea mjini huku wakilisukuma gari hilo.

Umati huo ulizidi kuongezeka na kufanya eneo lote la barabara hiyo kufungwa na umati wa watu vijana kwa wazee huku wakielekea kwenye mataa ya Magomeni, umati huo mara kadhaa  uliombwa  kupisha njia ili Sugu awahi ilishindikana hadi baada ya kuvuka mataa ya Magomeni gari liliposhika  barabara ya  kuelekea Kinondoni mpaka ulipofika kituo cha Hospitali ndipo Sugu alishuka kwenye gari hilo na kuwaomba watu wamruhusu ili awahi majukumu mengine, umati huo ulisikika ukimuhoji maswali kama vile "kwa unagombea Mbeya badala ya hapa?", baadaye umati huo ulimruhusu kuondoka huku ukilipuka kwa mayowe ya kumshangilia.Hali hiyo ilipelekea msongamano mkubwa wa magari kwa muda wa zaidi ya saa moja.

Friday, August 27, 2010

SUGU KUHUDHURIA JANGWANI NA HAFLA YA WANA MBEYA

Joseph Mbilinyi (Mr II SUGU)
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi leo jumamosi tarehe 28 Agosti, atakuwepo katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kitaifa, kisha jioni hii atahudhuri hafla ya kubadilishana mawazo ya Wana Mbeya na rafiki zao itakayofanyika kuanzia saa 1.00 jioni katika ukumbi wa Ballers Club - Namanga (zamani Shivas).

WASANII WASEMA WAO NA SUGU MPAKA MJENGONI

                                      Msanii wa Bongo Hip Hop - Mwanaharakati G Solo

Wasanii mbalimbali nchini wa muziki wa kizazi kipya na wa fani nyingine za muziki pamoja na sanaa kwa ujumla, wameahidi kupigana kufa na kupona kwa mbinu mbalimbali hata ikibidi maombi ili kuhakikisha msanii mwenzao Mr. II - SUGU anaingia bungeni (Mjengoni), wasanii hao ambao wameanzisha mtandao wa chini chini wamesema kuwa wanaamini jasiri ambaye ana uwezo wa kufikisha kilio chao kikasikika na kupatiwa ufumbuzi  ni Joseph.

 Msanii mmoja maarufu wa luninga ambaye amejipatia umaarufu mkubwa katika tasnia ya uigizaji nchini ambaye aliomba tusianike jina lake mpaka itakapofika wakati ambao watajitokeza hadharani alisema "hauwezi kuamini kuwa, japo tunaonekana na kupambwa na majarida mbalimbali na watu kudhania kuwa tuna mafanikio ya juu kifedha, lakini ukweli ni kwamba tunaishi kwa kuungaunga wakati watu wakitajirika kutokana na jasho letu", hivyo wasanii hao wanaamini jasiri ni Mr II - Sugu ambaye ameonekana sio muoga haswa linapokuja suala la kudai haki yake.

Taarifa hizi za wasanii zinakuja wakati ambapo baadhi ya wasanii wakiwemo Mkoloni wa kundi maarufu la Wagosi wa Kaya na G SOLO wakionekana kuwa bega kwa bega na Sugu katika harakati zake za kuhakikisha anaingia mjengoni. Huku hivi karibuni gwiji wa wa muziki wa Bongo Hip-Hop Joh Makini (Mwamba wa kaskazini) akiwa ameamua kuungana na Joseph Mbilinyi katika kampeni zake za kuwania Ubunge katika jimbo la Mbeya mjini.

JOSEPH MBILINYI (Mr II - SUGU) YUKO JIJINI


Baada ya uzinduzi wa kampeni zake Mbeya na kukusanya watu lukuki katika mikutano yake ya kampeni na kudhihirisha kuwa yeye ni "TUMAINI JIPYA KWA MAENDELEO YA WOTE" Mbunge mtarajiwa wa Mbeya Joseph Mbilinyi almaarufu kama SUGU sasa atakuwepo jijini kwa ajili ya muendelezo wa shughuli zake za harakati weekend hii, ambapo moja ya swala zito lililomleta ni kushiriki katika Uzinduzi wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Slaa (Silaha) katika viwanja vya jangwani siku ya jumamosi.

Joseph Mbilinyi ambaye siku za hivi karibuni amekuwa mwiba kwa wapindisha haki na wasiolitakia mema taifa hili pia atakuwepo jijini kwa ajili ya kuonana na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo pia atakuwa ni mmoja wa vijana atakayehudhuria katika usiku wa makutano ya watu wenye asili ya Mbeya, walioishi, waliosoma waliopita Mbeya pamoja na marafiki zao na wapenda maendeleo kwa ujumla katika siku ya Jumamosi tarehe 28 Agosti, kuanzia saa 1 jioni pale Ballers Club - Namanga au palipokuwa pakifahamika kama SHIVAS.


Mr. II amewataka wapenda maendeleo kwa ujumla na wanaomtakia mema yeye na taifa hili kuhakikisha wanaungana naye kwa namna moja ama nyingine katika kupigania maendeleo ya kweli ya taifa hili na siyo ya kufikirika na hakuna ujanja zaidi ya kushirikiana kuhakikisha sauti za kweli au wazalendo wenye uchungu na maendeleo ya taifa hili wanapewa nafasi ya kushika dola ili kumkomboa Mtanzania ambaye anasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa japo yeye ni maskini wa kutupwa.

Thursday, August 26, 2010

Mr II Sugu asema yeye si mwanasiasa

 Joseph Mbilinyi(Mr II - SUGU) hapo akisisitiza jambo kwa furaha

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Mbilinyi ‘Mr II Sugu’ amesema yeye si mwanasiasa kama anavyotazamwa na baadhi ya wanajamii bali ni mwanaharakati wa masuala ya maendeleo nchini.
Hayo aliyaeleza juzi, alipokuwa akirejesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Sugu alisema kuwa, harakati zake za kutetea jamii alizianza miaka 15 iliyopita kupitia tasnia ya sanaa ya uimbaji, hivyo kwa sasa anataka kuendeleza harakati hizo kupitia majukwaa ya siasa.
“Naomba nieleweke kuwa mimi si mwanasiasa, bali ukweli mimi ni mwanaharakati wa masuala ya maendeleo ya jamii na ninachokifanya sasa, ni kubadilisha jukwaa kutoka jukwaa la sanaa ya muziki na kutua katika jukwaa la siasa,’’ alisema Mbilinyi.
Aidha alipoulizwa na Tanzania Daima kuwa ni vitu gani anavyofikiri ni kipaumbele cha wananchi wa Jimbo hilo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Benson Mpesya, alikana kueleza kwa undani, kwa kile alichodai kuwa wakati wa kampeni ukifika, ndipo atakuwa na fursa ya kuyadadavua yale yote ambayo wananchi wamemweleza kutaka kusaidiana naye.
Mbilinyi alidokeza kuwa kitu kinachomkera zaidi ni siasa za makundi ambazo zinaendelea kulizorotesha kimaendeleo jimbo hilo, ambalo kihistoria ni lenye neema lakini ni jimbo pekee duniani ambalo halina barabara licha ya kuitwa jiji.
“Nakerwa sana na siasa za makundi zinazoendelezwa na baadhi ya viongozi waliopo madarakani, lakini niwe wazi kuwa, nimewahi kuimba wimbo unaohusu Mbeya na maisha ya watu wake, lakini ukweli ni kwamba nina mapenzi mema na Mbeya zaidi ya kuuimbia nyimbo,’’ alisema Sugu.
Awali Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema kuwa, kuchukua fomu kwa Mbilinyi siyo tiketi ya kumsimika kupeperusha bendera ya chama hicho, bali hatima ya kumpata atakayepeperusha bendera ya chama hicho itakuwa Julai 24 mwaka huu, ambako hadi sasa wengine waliojitokeza kuomba ridhaa hiyo ni Gwakisa Mwakasendo, Eddo Makata na Daudi Mponzi.

Mr. II - From Wikipedia, the free encyclopedia
Joseph Mbilinyi, known for his stage names Mr. II and Sugu and 2-proud, is one of the founders of the hip hop music scene in Tanzania. He has travelled around the world performing. He's respected among his peers for his outstanding contribution to helping the music business find its own direction. Mr. II was stems from Songea in Southern Tanzania, started to rap in 1990, in his youth when he was still in school. His inspirations were Ice Cube, Niggers With Attitude and above all Tupak Shakur. Mr. II was the first Tanzanian rap artist to have major success with his music. Through his music and language he express and addresses politics, social inequalities and other problems that affected Tanzanians. Most would consider his music as a voice for the voiceless, his brand of rap is soulful, lyrical, rhythmical and from the heart. This is because Mr. II is not afraid to tell it like it is, undertaking sensitive issues of concern to many Tanzanians such as democracy, child prostitution, police brutality and corruption.[1] He became so popular that his music reached audiences even in rural areas where rap had not been heard before. Due to the quality of his music and the message in his music, older people were more acceptance to his music and contributed to making him the first Tanzanian rapper to have a mainstream hit. Also making Mr II the M-Net Best Male Artist Grammy Award Winner for Tanzania in 2001.Mr. II is East Africa’s most popular Bongo Flava icon, and through this genre he was able to make a difference and create opportunities for the youth. [2]

Style and Message

Sugu, which loosely translates to 'Stubborn' or 'Hard', has been just that in terms of his popular longevity. With over a decade of success, Sugu has maintained his rebellious persona as a social outcast. Performing in Swahili, Sugu addresses social issues that plague both urban and rural East Africans. His socially conscious lyrics touch on issues ranging from prostitution to immigration to the plight of street children. [3] Examples of his politically charged music is apparent in the songs Hali Halisi,[1] (real situation) in which he depicts the struggles of street life, and the oppressive conditions of the government, prisons, and judicial system.
"Everyday is us against the police and the police against us
The judge at the court is waiting for us
The prison officer is waiting for us[4] "
His lyrical style which is methodic yet quick has been mimicked by many of the genre’s newcomers. His peers view “his observant narratives, canny wordplay and flamboyant delivery” [5] as a trademark of their genre.
Mr. II is an outspoken advocate of Tanzanian hiphop or Bongo Flava.
Sugu has seen success in various realms of the African Hip Hop scene. He is the primary organizer of the annual Tanzania Hip-Hop Summit, a yearly convention of East Africa’s most prominent and up-and-coming music stakeholders. The summit is held in Dar-es-Salaam in December and brings together everyone from artists to producers to TV representatives.[3] He was also the publisher of Deiwaka, a music and arts magazine that is no longer in print. Sugu is one of the most recognizable artists in the world of East African Hip-hop, has won numerous Pan-African music awards and has performed at a number of international festivals. [6] Regardless of his efforts to differentiate himself and his genre, Mr. II continues to be compared to the many great Hip-Hop artists from the U.S such as Nas, Jay-Z or Run DMC. [2] [5]
Mr. II's song "Haki" has been hailed as the "definitive bongoflava anthem" In Swahili Haki means freedom and justice[7] Mr. II's lyrics address themes that are typical of Bongoflava. Bongoflava "tackle[s] subjects faced by the continent and the world over: poverty, ambition, success, money, HIV/AIDS"[8]
Sugu is also the Founder and Director of DEIWAKA ENTERTAINMENT CO. LTD...A company that has dedicated itself in promoting and developing Tanzanian hiphop/Bongoflava as part of helping in the fight against poverty and unemployment problems among youths in Tanzania.
At the 2005 Tanzania Music Awards his album Moto Chini was nominated in the best Hip Hop Album category [9].

Discography

Mr II is the most productive Tanzanian hip hop musician, given the number of released albums:
  • Ni Mimi (1995)
  • Ndani ya Bongo (1996)
  • Niite Mister II (1998)
  • Nje ya Bongo (1999)
  • Millennium (2000)
  • Muziki na Maisha (2001)
  • Itikadi (2002)
  • Sugu (2004)
  • Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006)
  • VETO (2009)

Welcome to the Online Home of East Africa's hip hop legend, SUGU a.k.a Mr II.Firstly, sincere apologies to those who have long-awaited this site. It is still under-development but after withholding it for so long, and as a reward to those who have been patient, we now have the pleasure of giving you a taster of whats to come when its completed. This website is still being developed to properly present you an insight into this legendary talent and promote his latest self-titled album.
SUGU is without question amongst the most popular and successful hip-hop artists representing Tanzania (aka 'Bongo'). He is a much respected figure in the East African hiphop scene and has over a decade of years in the game to his credit.
Some remember him as 2 Proud back in the early 90's, others still call him Mr 2 or Mr II, but SUGU is now the new name of this legend. A man of the people, a voice of the voiceless, he has never been afraid to say it as it is so always tells it as it is.
His style is best described as lyrical, soulful, rhythmical and straight from the heart. His tight and articulate Swahili flow is remarkable and the manner in which he handles a multitude of subject matters is engaging even to those who may not understand his Swahili narratives.
With various attached accolades and now 8 domestically acclaimed albums already to his name, he is synonymous with East African Hip-hop and widely accredited to really motivating the hiphop scene in Tanzania and popularising the phrase 'Bongo Flava' - an endearing name given to local urban music of Tanzanian origin.

(Habari zilizopita) Mr II kuibeba Chadema Ubunge Mbeya Mjini


Pichani katika ni Mwanamuziki muasisi wa Bongo fleva nchini Mr 2 (Sugu) akionyesha kitambulisho kwa kutambulika rasmi kuwa mwanachama wa chama cha Chadema.Kushoto kwake ni Bw John Mnyika wa Chadema aliyemkabidhi Mr 2 Kitambulisho hicho.

Brandy Nelson

MSANII mkongwe wa  muziki wa kizazi kipya, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr II, ameteuliwa kuiwakilisha Chadema kugombea ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini baada ya kushinda kwenye kura za maoni.

Mbilinyi alichaguliwa jana kwednye mkutano wa kura za maoni zilizopigwa na wanachama wa chama hicho jijini  Mbeya.

Akitangaza matokeo ya kura hizo, msimamizi wa kura za maoni wa Chadema, Sambwee Shitambala alisema mgombea huyo ameshinda baada ya kupata kuwa kura 175 ambazo ni sawa na asilimia 48.3 ya kura 362 zilizopigwa.

 Shitambala, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema mkoani Mbeya, alisema Mbilinyi alimshinda mpinzani wake kwa tofauti ya kura 53. Mpinzani huyo, Daud Mponzi alipata kura 122.

Mgombea mwingine ambaye ni mwandishi wa habari, Christopher Nyenyembe alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 54 na Gwakisa Mwakasendo aliambulia kura tisa.

Mapema, Shitambala aliwataka wajumbe wa mkutano huo kumchagua mtu mwenye sifa, anayekubalika na anayeuzika kwa kuzingatia hali ya kisiasa katika Jimbo la Mbeya Mjini  ili Chadema iweze kuibuka na ushindi.

Shitambala  ambaye pia ni mgombea wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini, alisema katibu mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Peter Slaa amempigia simu na kumtaka awaeleze wanachama hao kuchagua mtu makini.

Kabla ya uchaguzi, mwanachama mmoja alimtaka Mbilinyi aeleze namna atakavyofanya ili kukiwezesha chama hicho kuwa na ofisi nzuri kuanzia ngazi ya kata.

Akijibu swali hilo, Mr ll alisema ubunge wake utakuwa shirikishi kwa wanachama wote na kuwa atajitahidi kutafuta wafadhili wa kusaidia ujenzi wa ofisi hizo.

Sugu amekuwa mtetezi mkubwa wa haki za wasanii nchini akipinga ukandamizaji unaofanywa na baadhi ya wamiliki wa vituo vya redio nchini, mameneja na makampuni.

Sugu alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza wa muziki wa rap ya Kitanzania kujizolea mashabiki wengi, kiasi cha kufuatwa na lundo la watu kila alipoonekana hadharani.

Lakini baada ya kukorofishana na baadhi ya makamapuni ya muziki alianza kutoweka kutokana na nyimbo zake kutopewa nafasi kwenye vipindi vya redio na televisheni.

(Habari zilizopita) MKASA WA MR II HAKI AU UONEVU


Bila shaka umezipata habari ambazo zimeshaenea sehemu mbalimbali ulimwenguni kuhusu kukamatwa na kisha kuachiwa kwa dhamana(kajiwekea mwenyewe mdhamana)Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Joseph Mbilinyi aka Mr. II alias Sugu.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo blogs ya Issa Michuzi na Da,Subi(wavuti dot com) sababu za kukamatwa kwake leo na maafisa wa jeshi la Polisi akiwa katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa kikao cha kuongelea masuala ya muziki, ni kufuatia mmoja wa viongozi wa kituo kimoja  cha redio ya jijini Dar Es Salaam kumshitaki kuwa anamtishia maisha kwenye wimbo mmoja ambapo Mr. II anasikika akisema “I wanna kill you”. Wimbo huo na nyinginezo zinapatikana katika albamu ya ‘Anti-Virus’ inayosambazwa bure mtaani.
Katika utetezi wake,Mr. II ambaye alitarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania Ubunge mkoani Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA,anasema jambo hilo limemshangaza kwa kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo ni ya kisanii zaidi na yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja.
Amedai alikamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo kwa saa kadhaa na kisha kuachiwa kwa dhamana ya kujidhamini mwenywe, na ametakiwa kuripoti kituoni hapo kesho kutwa.
Mr. II pamoja na wasanii wengine wamerekodi nyimbo kadhaa na kuweka kwenye albamu moja ambayo wameiita Anti-Virus, wakielezea hisia zao mbalimbali za kimaisha na kadhia la muziki wa Tanzania.
Je,hii na haki na sahihi(kwa Sugu kufikishwa katika mkono wa sheria)  au ni uonevu? Ni kweli kwamba inawezekana Sugu amekamatwa kutokana na juhudi zake mpya katika ulimwengu wa siasa ambapo hivi karibuni yeye na baadhi ya wasanii walitangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)?

Wednesday, August 25, 2010

SUGU AFUNIKA MBEYA


Na Mwandishi Wetu, Mbeya
 
Mgombea Ubunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amefunika katika mkutano wake wa kwanza wa kujinadi.

Sugu, alivuta umati mkubwa na kuweka historia Mbeya kuwa mgombea wa kwanza wa ubunge katika historia kwa kuitikiwa na idadi kubwa ya watu.

Mwandishi wetu ambaye alihudhuria mkutano huo uliochukua nafasi kwenye Viwanja vya Rwanda Nzovwe vilivyopo eneo la Mama John, Mbeya Jumamosi iliyopita, aliweza kuifananisha sura iliyokuwepo na ile ambayo hujiri Viwanja vya Jangwani katika mikutano ya kitaifa.

Katika uzinduzi huo, wasanii wakubwa wa Muziki wa Kizazi Kipya, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G-Solo’ na Danny Msimamo walitoa shoo iliyosisimua na kuufanya mkutano utawaliwe na shamrashamra.

Sugu alipopanda jukwaani kuzungumza na wananchi, alitumia dakika 45 ambapo baadhi ya wananchi walimsikiliza kwa utulivu lakini mara nyingi walikuwa wakilipuka na kumshangilia kwa nguvu.

Baadaye mwandishi wetu alipozungumza na Sugu, alisema: “Umeona mwenyewe, ndiyo tumezindua, hapa tutapiga mikutano kujinadi na hakuna kulala mpaka kieleweke. Umati huu unatosha kukufanya uone jinsi ninavyokubalika.

“Mbeya ni nyumbani, shida za hapa nazijua na nimeamua kuja kusimama kutetea kwetu. Hakuna kulala kaka.”

NATAKA SUGU ASHINDE UBUNGE MBEYA

WARAKA MUHIMU
NATAKA SUGU ASHINDE UBUNGE MBEYA
Na Ezekiel Kamwaga

Miezi michache iliyopita niliiona picha ya msanii maarufu wa muziki nchini, Ambwene Yesayah (AY), akimchangia kiasi cha sh 100,000 Mwanahabari Violeth Mzindakaya, kumsaidia kuwania ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu.Wakati huo, taarifa kwamba msanii mwingine wa muziki, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Mr II naye alikuwa mbioni kuwania ubunge hazikuwa wazi.
Kwa hiyo nilielewa hatua hiyo ya AY. Wanahabari wamefanya kazina wasanii wa fani mbalimbali. Na pengine AY aliona Mzindakaya anaweza kuwa msaada kwao kwa vile amefanya nao kazi na anafahamu shida zao.
Hata hivyo, sasa katika kipindi ambacho Mbilinyi ametangaza kuwa atawania ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nafikiri wasanii wanapaswa kumuunga mkono, ili apate nafasi hiyo.
Duniani kote, hasahasa katika nchi zilizoendelea, makundi mbalimbali huhakikisha kuwa yana uwakilishi wao bungeni. Na hili pia,kwa kiasi fulani lipo hapa kwetu.Bunge la Tanzania lina wabunge wa viti maalumu wanaowakilisha makundi mbalimbali nchini, kuanzia vijana, walemavu, wakinamama na vyuo vya elimu ya juu.
Mbilinyi anakuja na sura mpya katika uwakilishi huu, yeye atawakilisha vijana wanaoishi kwa kutegemea muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva.Katika hali ya kawaida wasanii wa Tanzania wanahitaji mwakilishi wao ndani ya Bunge letu tukufu. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, muziki wa Bongo fleva umekuwa miongoni mwa vyanzo vikubwa vya ajira hapa nchini.
Ajira kwa vijana imepunguza baadhi ya matatizo ambayo yangeikumba jamii ya watanzania iwapo vijana hawa wangeamua kufanya vitendo vingine.Nimesikia nyimbo nyingi za vijana hawa wakizungumzia namna muziki ulivyowaokoa kutoka kuwa majambazi, wabakaji na mateja. Nafikiri imefika wakati tunahitaji kuuheshimu muziki huu. Ndio maana nadhani ni muhimu kwa muziki huu kuwa na mtu wa kuusemea ndani ya chombo cha kutunga sheria na kuisimamia serikali.
Kilio cha wasanii kuhusu hakimiliki na unyanyasaji na unyonyaji unaofanywa kwa wanamuziki na wasanii Tanzania kitapata nguvu iwapo atakuwapo mtu wa kuwasemea bungeni. Binafsi kama ningeambiwa ni msanii gani wa Tanzania ningetamani apewe fursa ya kuingia Bungeni bila shaka ningemtaja Mr. II.
Nimesikia nyimbo zake kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita na amekuwa na ujumbe ambao unaeleza maisha halisi ya Mtanzania. Ameimba kuhusu namna umasikini unavyowaathiri Watanzania , ubaya wa uongozi bora na ameipigania fani ya muziki isionekane kuwa ya kihuni .
Ameitafuta haki ya kuwa mwakilishi wa wasanii wa Tanzania kutokana na rekodi ya kutetea haki zao kila wakati na kila mara.Nafahamu kwamba ndani ya bunge lililopita, alikuwapo John Komba ambaye sote tunafahamu ni msanii na alipaswa awe mtetezi wao Bungeni.
Tatizo langu na Komba ni kuwa yeye ni mtu wa kikazi tofauti na vijana wanaoishi kwa kutegemea Bngo fleva. Tangu miaka ya nyuma, yeye amekuwa kaitumika ndani ya chama na serikali. Hajawahi kusota katika namna ambayo wakina Mr. II walisoka katika siku za nyuma.
Hata kama albamu ya kundi lake la Tanzania One theatre (TOT) isipouza vizuri sokoni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitahakikisha wafanyakazi wake wanalipwa mishahara yao kama kawaida.Kama albamu ya Diamond, Ngwair, Juma nature, Afande Sele, Lady JD, Profesor Jay, Ray C isipouza sokoni, hiyo inakuwa “imekula kwake”. Hawa hawana mjomba wa kuwalipa mshahara.
Ndio maana naamini wasanii wa Tanzania watafaidika sana na kuwakilishwa na mmoja wao kuliko kuwakilishwa na mtu mwingine.Huwezi kutarajia mbunge wa kundi la vijana akaenda kuwatetea wasanii kama ambavyo Mr. II atafanya. Si lazima mtu akiwa kijana basi ni lazima ajue kila tatizo linalowakumba wasanii.
Mbaya zaidi, wengi wabunge vijana wanaopata fursa katika siku za hivi karibuni, hupata nafasi hiyo ama kwa sababu ya kuwa “watoto wa wakubwa” au watu wanaotumwa na vigogo kwenda kuwawakilisha .Hawa hawana sababu ya kupaza sauti kuwatetea wasanii .hawa wanajua ni Baba ama Mama zao waliowafikisha hapo. Wawatetee au wasiwatetee wasanii, haitabadili chochote kwao.
Ningependa kuona wasanii wa Tanzania wakiungana kwa pamoja kumuunga mkono Joseph Mbilinyi kama kweli wanataka sauti zao zisikike kwa pamoja.Kama wanataka mtu azungumze kile wanachokitaka, kwa lugha yao na kwa namna yao, Mr II ndiye anayefaa.
Matukio ya karibuni zaidi yameonyesha kwamba Mr II haogopi mtu yeyote pale anapoona haki yake au ya wasanii wenzake zinaporwa na yeyote.Ninajua kwamba wapo watakaowaambia wasanii wasimuunge mkono Mr. II kwa vile anawania nafasi hiyo kupitia chama cha upinzani. Huu ni upuuzi mtupu.
Raisi mstaafu, Benjamin Mkapa, alipata kutamka katika siku za nyuma kwamba rangi ya paka haina maana yoyote isipokuwa uwezo wake wa kukamata panya wanaosumbua nyumbani.Kama paka anafanya kazi yake vyema, awe mweusi, mweupe au mwekundu haina maana yeyote. Wanachohitaji wasanii ni mtu wa kuwawakilisha Bungeni na si chama ca siasa.
Ningetamani kuona wasanii wa Tanzania wakifanya onyesho la pamoja katika jimbo la Mbeya Mjini kutangaza kumuunga mkono Joseph.Ningetaka kuona wasanii wa Tanzania wakihakikisha wako pamoja na Mr. II wakati wa kampeni kwa kupokezana ili kuhakikisha hakuna hata kipindi kimoja ambapo anabaki mwenyewe jukwaani.
Ninafahamu kwamba Mr. II hatajali sana kama ataachwa mwenyewe na wasanii wetu ambao watakuwa wakikimbizwa huku na huko na wanasiasa watakaotaka kutumia ushawishi wao katika kipindi hiki cha uchaguzi.Jambo la muhimu kwa msanii yeyote ili kushinda katika maisha haya ni kuwa na uwezo wa kusimama mwenyewe. Na Joseph amesimama mwenyewe katika miaka yake 15 ya fani hii.
Lakini kwa faida ya wasanii wa nchi yetu, kizazi cha sasa na kijacho, nadhani huu ni wakati muafaka wa kumuunga mkono mtu mmoja tuu …....... Joseph Mbilinyi A.k.a SUGU.

Tuesday, August 24, 2010

BLOG HII NI MPYA (IKO KWENYE MATENGENEZO)

Tunakukaribisha uungane nasi katika harakati za kuhakikisha Mr II sugu anaingia bungeni ili kuendeleza harakati za kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye matatizo ambayo yanamkabili kwa ajili ya uroho wa wachache.

 TUNAHITAJI MCHANGO WAKO WA HALI NA MALI ILI KUHAKIKISHA TUNAFANIKIWA

KARIBUNI - Tutatangaza njia za kutuma mchango wako kwa Joseph Mbilinyi (Mr II SUGU) ili kumsaidia katika kampeni

SUGU YUKO TAYARI KWA MAPAMBANO

Mwanaharakati JOSEPH MBILINYI (MR II SUGU) katika posters ya kampeni ya kugombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini, hapo ni KIKAZI ZAIDI!

Monday, August 23, 2010

Kwa nini nimeanzisha Blog?

Mimi ni Joseph Mbilinyi aka SUGU, Mr II, au zamani 2 Proud. Ni ndugu yenu na mwenzenu.
Nimeanzisha Blog ili kupata maoni na mapendekezo mbalimbali katika mapambano yangu. Nilikuwa mwanaharakati kwa muda mrefu kupitia muziki na sasa nimeamua kuendeleza harakati kwa style nyingine ya siasa maana wanasema "aliye juu mngoje chini" na nimesubiri sana chini lakini nikaona ni bora niende hukohuko juu na labda nitasikilizwa.
Nimeanzisha Blog ili nipate ushirikiano kwa ndugu zangu toka pande zoote za dunia ili tusaidiane kuiendeleza Mbeya na Tanzania yetu kwa ujumla ambayo inatuhitaji sisi, ningependa sana vijana tuchangamke na kupambana ili Tanzania yetu ikae sawa na tuendelee katika kila nyanja ya kipato, kielimu na kiafya na mambo mengine.
Naomba ushirikiano wenu ndugu zangu.