Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Wednesday, August 25, 2010

SUGU AFUNIKA MBEYA


Na Mwandishi Wetu, Mbeya
 
Mgombea Ubunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amefunika katika mkutano wake wa kwanza wa kujinadi.

Sugu, alivuta umati mkubwa na kuweka historia Mbeya kuwa mgombea wa kwanza wa ubunge katika historia kwa kuitikiwa na idadi kubwa ya watu.

Mwandishi wetu ambaye alihudhuria mkutano huo uliochukua nafasi kwenye Viwanja vya Rwanda Nzovwe vilivyopo eneo la Mama John, Mbeya Jumamosi iliyopita, aliweza kuifananisha sura iliyokuwepo na ile ambayo hujiri Viwanja vya Jangwani katika mikutano ya kitaifa.

Katika uzinduzi huo, wasanii wakubwa wa Muziki wa Kizazi Kipya, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G-Solo’ na Danny Msimamo walitoa shoo iliyosisimua na kuufanya mkutano utawaliwe na shamrashamra.

Sugu alipopanda jukwaani kuzungumza na wananchi, alitumia dakika 45 ambapo baadhi ya wananchi walimsikiliza kwa utulivu lakini mara nyingi walikuwa wakilipuka na kumshangilia kwa nguvu.

Baadaye mwandishi wetu alipozungumza na Sugu, alisema: “Umeona mwenyewe, ndiyo tumezindua, hapa tutapiga mikutano kujinadi na hakuna kulala mpaka kieleweke. Umati huu unatosha kukufanya uone jinsi ninavyokubalika.

“Mbeya ni nyumbani, shida za hapa nazijua na nimeamua kuja kusimama kutetea kwetu. Hakuna kulala kaka.”

No comments:

Post a Comment