Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Thursday, August 26, 2010

(Habari zilizopita) MKASA WA MR II HAKI AU UONEVU


Bila shaka umezipata habari ambazo zimeshaenea sehemu mbalimbali ulimwenguni kuhusu kukamatwa na kisha kuachiwa kwa dhamana(kajiwekea mwenyewe mdhamana)Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Joseph Mbilinyi aka Mr. II alias Sugu.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo blogs ya Issa Michuzi na Da,Subi(wavuti dot com) sababu za kukamatwa kwake leo na maafisa wa jeshi la Polisi akiwa katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa kikao cha kuongelea masuala ya muziki, ni kufuatia mmoja wa viongozi wa kituo kimoja  cha redio ya jijini Dar Es Salaam kumshitaki kuwa anamtishia maisha kwenye wimbo mmoja ambapo Mr. II anasikika akisema “I wanna kill you”. Wimbo huo na nyinginezo zinapatikana katika albamu ya ‘Anti-Virus’ inayosambazwa bure mtaani.
Katika utetezi wake,Mr. II ambaye alitarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania Ubunge mkoani Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA,anasema jambo hilo limemshangaza kwa kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo ni ya kisanii zaidi na yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja.
Amedai alikamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo kwa saa kadhaa na kisha kuachiwa kwa dhamana ya kujidhamini mwenywe, na ametakiwa kuripoti kituoni hapo kesho kutwa.
Mr. II pamoja na wasanii wengine wamerekodi nyimbo kadhaa na kuweka kwenye albamu moja ambayo wameiita Anti-Virus, wakielezea hisia zao mbalimbali za kimaisha na kadhia la muziki wa Tanzania.
Je,hii na haki na sahihi(kwa Sugu kufikishwa katika mkono wa sheria)  au ni uonevu? Ni kweli kwamba inawezekana Sugu amekamatwa kutokana na juhudi zake mpya katika ulimwengu wa siasa ambapo hivi karibuni yeye na baadhi ya wasanii walitangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)?

No comments:

Post a Comment