Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Friday, August 27, 2010

WASANII WASEMA WAO NA SUGU MPAKA MJENGONI

                                      Msanii wa Bongo Hip Hop - Mwanaharakati G Solo

Wasanii mbalimbali nchini wa muziki wa kizazi kipya na wa fani nyingine za muziki pamoja na sanaa kwa ujumla, wameahidi kupigana kufa na kupona kwa mbinu mbalimbali hata ikibidi maombi ili kuhakikisha msanii mwenzao Mr. II - SUGU anaingia bungeni (Mjengoni), wasanii hao ambao wameanzisha mtandao wa chini chini wamesema kuwa wanaamini jasiri ambaye ana uwezo wa kufikisha kilio chao kikasikika na kupatiwa ufumbuzi  ni Joseph.

 Msanii mmoja maarufu wa luninga ambaye amejipatia umaarufu mkubwa katika tasnia ya uigizaji nchini ambaye aliomba tusianike jina lake mpaka itakapofika wakati ambao watajitokeza hadharani alisema "hauwezi kuamini kuwa, japo tunaonekana na kupambwa na majarida mbalimbali na watu kudhania kuwa tuna mafanikio ya juu kifedha, lakini ukweli ni kwamba tunaishi kwa kuungaunga wakati watu wakitajirika kutokana na jasho letu", hivyo wasanii hao wanaamini jasiri ni Mr II - Sugu ambaye ameonekana sio muoga haswa linapokuja suala la kudai haki yake.

Taarifa hizi za wasanii zinakuja wakati ambapo baadhi ya wasanii wakiwemo Mkoloni wa kundi maarufu la Wagosi wa Kaya na G SOLO wakionekana kuwa bega kwa bega na Sugu katika harakati zake za kuhakikisha anaingia mjengoni. Huku hivi karibuni gwiji wa wa muziki wa Bongo Hip-Hop Joh Makini (Mwamba wa kaskazini) akiwa ameamua kuungana na Joseph Mbilinyi katika kampeni zake za kuwania Ubunge katika jimbo la Mbeya mjini.

No comments:

Post a Comment