Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Friday, August 27, 2010

JOSEPH MBILINYI (Mr II - SUGU) YUKO JIJINI


Baada ya uzinduzi wa kampeni zake Mbeya na kukusanya watu lukuki katika mikutano yake ya kampeni na kudhihirisha kuwa yeye ni "TUMAINI JIPYA KWA MAENDELEO YA WOTE" Mbunge mtarajiwa wa Mbeya Joseph Mbilinyi almaarufu kama SUGU sasa atakuwepo jijini kwa ajili ya muendelezo wa shughuli zake za harakati weekend hii, ambapo moja ya swala zito lililomleta ni kushiriki katika Uzinduzi wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Slaa (Silaha) katika viwanja vya jangwani siku ya jumamosi.

Joseph Mbilinyi ambaye siku za hivi karibuni amekuwa mwiba kwa wapindisha haki na wasiolitakia mema taifa hili pia atakuwepo jijini kwa ajili ya kuonana na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo pia atakuwa ni mmoja wa vijana atakayehudhuria katika usiku wa makutano ya watu wenye asili ya Mbeya, walioishi, waliosoma waliopita Mbeya pamoja na marafiki zao na wapenda maendeleo kwa ujumla katika siku ya Jumamosi tarehe 28 Agosti, kuanzia saa 1 jioni pale Ballers Club - Namanga au palipokuwa pakifahamika kama SHIVAS.


Mr. II amewataka wapenda maendeleo kwa ujumla na wanaomtakia mema yeye na taifa hili kuhakikisha wanaungana naye kwa namna moja ama nyingine katika kupigania maendeleo ya kweli ya taifa hili na siyo ya kufikirika na hakuna ujanja zaidi ya kushirikiana kuhakikisha sauti za kweli au wazalendo wenye uchungu na maendeleo ya taifa hili wanapewa nafasi ya kushika dola ili kumkomboa Mtanzania ambaye anasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa japo yeye ni maskini wa kutupwa.

No comments:

Post a Comment