Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Sunday, August 29, 2010

SUGU ALISIMAMISHA JIJI KWA MUDA

             Umati wa watu ukilisukuma gari alilopanda Joseph Mbilinyi (Mr II - Sugu).

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya na mwanaharakati Joseph Milinyi (Mr II - SUGU) ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Mbeya mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ameshangaza jiji baada ya lundo la watu kumsindikiza kwa kusukuma gari alilokuwemo baada ya kutoka jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni wa CHADEMA kitaifa.

SUGU ambaye alivuta hamasa ya watu wengi waliohudhuria uzinduzi huo alikuwa ni mmoja wa watu waliopanda jukwaani kuhamasisha na alitumia kipaji chake kutoa ujumbe kupitia baadhi ya nyimbo ambazo zilimchukulia umaarufu mkubwa alizotoa miaka ya nyuma.

Baada ya mkutano umati wa watu ulimzuia kuingia kwenye gari hadi alipoongea nao na kuwasihi wamruhusu kwenda sababu kuna kikao anawahi, baada ya kupanda gari hilo ambalo kulikuwa na wasanii wengine, Wanaharakati Mkoloni, G Solo na Dan Msimamo wananchi walianza kulisukuma huku wakipiga mayowe kumshangilia na huku wakiimba kwa vionjo  mbalimabali, ikiwemo kiitikio "Sugu, tumemuona Mbunge wa Mbeya" walilisukuma gari hilo mpaka walipoingia barabara ya Morogoro eneo la jangwani na kuzuia magari yote yaliyoyakitokea mjini huku wakilisukuma gari hilo.

Umati huo ulizidi kuongezeka na kufanya eneo lote la barabara hiyo kufungwa na umati wa watu vijana kwa wazee huku wakielekea kwenye mataa ya Magomeni, umati huo mara kadhaa  uliombwa  kupisha njia ili Sugu awahi ilishindikana hadi baada ya kuvuka mataa ya Magomeni gari liliposhika  barabara ya  kuelekea Kinondoni mpaka ulipofika kituo cha Hospitali ndipo Sugu alishuka kwenye gari hilo na kuwaomba watu wamruhusu ili awahi majukumu mengine, umati huo ulisikika ukimuhoji maswali kama vile "kwa unagombea Mbeya badala ya hapa?", baadaye umati huo ulimruhusu kuondoka huku ukilipuka kwa mayowe ya kumshangilia.Hali hiyo ilipelekea msongamano mkubwa wa magari kwa muda wa zaidi ya saa moja.

No comments:

Post a Comment