Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Sunday, June 14, 2015

MBUNGE "SUGU" AIBUKIA KISIWANI MAFIA

• AFANIKIWA KUTOA VIONGOZI WA CHADEMA POLISI
• ATEMBELEA VIJIWE NA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA


Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA Joseph O. Mbilinyi "Sugu" wikiendi hii alikuwa kwenye ziara ya ujenzi wa Chama kwenye kisiwa cha Mafia na kufanikiwa kufanya mambo kadha wa kadha ya ujenzi wa Chama. 

Katika ziara yake hiyo ambayo licha ya kutembelea vijiwe mbalimbali na kubadilishana mawazo na wakazi wa kisiwa hicho pia alikumbana na mkasawa kushikiliwa kwa viongozi wa CHADEMA kisiwani hapo kwa makosa yasioeleweka ambapo kikosi hicho cha Mbunge huyo wa Mbeya waliweza kupigania mpaka usiku wa manane kuhakikisha viongozi hao wanatolewa polisi.

Pia katika ziara hiyo Mbunge pia aliweza kuongea na viongozi wa Kata katika jimbo hilo la Mafia pamoja na kusalimiana na vijana wa kikosi cha Red Brigade katika kisiwa hicho pamoja na kusaini kadi nyingi za CHADEMA ambazo wakazi wa kisiwa hicho walikuwa wakizihitaji kwa udi na uvumba. 

Baadaye jumapili aliweza kuongea na wakazi wa kisiwa hicho kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani hapo na kusisitiza elimu ya uraia ikiwemo kutoogopa vitisho vya polisi ambao ni vibaraka wa chama tawala.

Mbunge huyo pia alivutiwa na mandhari tulivu ya kisiwa hicho na huku akiwa amefikia katika chumba ambacho akina AC wala TV ambapo kwa madai yake alisema ni kizuri kwa utulivu na kutafakari.

No comments:

Post a Comment