Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, September 3, 2011

ZIARA YA MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI KUELEKEA MAENEO TOFAUTI YA JIJINI MBEYA

HATUA YA KWANZA ( ENEO LA UJENZI )

 Wakati anaianza Safari ya kuelekea Eneo la Iziwa Kukagua Miradi ya Maendeleo Joseph Mheshimiwa Mbilinyi alipata Ujumbe kutoka kwa vijana wanaofanya kazi ya Kuosha Magari eneo la Ujenzi(Sinde) Jijini Mbeya ambao wanadai wamekatazwa kufanya Kazi zao Eneo hilo, hivyo ikamlazimu kufika kwa Vijana hao na kuwasikiliza mara moja kabla ya kuendelea na Safari
                    
                                              Akiwasikiliza kwa Umakini maelezo yao

Vijana hao wanadai awali walipo ruhusiwa kufanya kazi zao eneo hilo waliamuliwa kuchimba shimo ili kutunza Maji machafu yasizagae ovyo, nao waliitikia wito kama inavyoonekana.


Baadae wakaambiwa watafuta Zana za kufanya eneo hilo liwe la kisasa, Mchanga na Mawe vipo tayari kama vinavyoonekana lakini hajapewa kibali cha keundelea na Ujenzi

Mama Ntilie nao kilio chao ni Biashara yao kwa sasa haiendi vizuri kutokana na Kukosa wateja, ambao tegemeo lao kubwa ni uoshaji wa Magari.

Sugu wa Vijana, Sugu wa Wazee, Sugu wa Watoto, Sugu kwa kila Mtu, Sugu kwa Maendeleo ya Mbeya..., Ukaribu kwa kila Mtu ndiyo Jadi yake.

Alichukua Vielelezo vinavyoonesha kuwa Wanalipia Ushuru eneo hilo lakini hawaruhusiwi kufanya Kazi na Kuwaahidi kuwa atalipeleka kwa Mkurugenzi wa Jiji ili waweze kutatua Mgogoro huo.




HATUA YA PILI (ENEO LA IZIWA)

Mheshimiwa Mbunge Mguu kwa Mguu na katibu wake bwana Fredrik Maliki walipo fika  Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Iziwa 

Akitia Sahihi kitabu cha Wageni Ofisi ya Afisa Mtendaji.

Mh kipata Maelezo Mafupi kutoka kwa Afisa Mtendaji kabla ya kwenda kukagua Miradi ya Maendeleo

Mbunge Kazini...., Akikagua Ufyatuaji wa Matofali kwa Ajili ya Ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Iziwa ambayo ni kati ya miradi anayo pamba na ikamilike haraka ili kuboresha huduma xya afya katika eneo 

"Mheshimiwa Eneo loote hadi kule ni la Zahanati, hivyo tuna mpango wa kujenga Nyumba ya Daktari na Majengo mengineyo.!" Afisa Mtendaji wa Kata ya Iziwa Bwana Samwel Mboya akimpa Maelezo Mheshimiwa Sugu


Ati hili ni Jiwe la Msingi kama Linavyosomeka

Jengo la Zahanati hiyo upande wa Nyuma

Ukaguzi makini, Mh.Sugu akikagua Vyoo ambavyo hakuridhishwa navyo na kutaka Uongozi wa Kata ushirikiane naye kuhakikisha kila Kitu kiende sawa kukamilisha ujenzi huu.


Sehemu ya kuchoma Taka za Zahanati hiyo

Muonekano wa Hospitali hiyo kwa Mbali kidogo



        HATUA YA TATU ( KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI IZIWA )

Mh. Sugu na Afisa Mtendaji


Akielekea Ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ili kupata Maelezo na Kufahamu changamoto gani zina wakabili ili waweze kushirikiana kuzitatua.

"Karibu sana Mheshimiwa, ni Viongozi wachache sana wenye Moyo kutembelea Mazingira kama haya.!! Umeweka Historia"- Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Iziwa Ndugu G.D Golenimali

Karibu sana Mheshimiwa Sugu, alielezwa kuna Upungufu wa Walimu 20 na Nyumba za Walimu hivyo tunaomba Msaada wako.!


                                         
                                       
                                  Sugu akitoa Salam kwa Wanafunzi wa Darasa la Saba shule ya Msingi Iziwa.
Mh akiwa kwenye Eneo la Nyumba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Iziwa
Akioneshwa nafasi ya Kujenga nyumba nyingine za Walimu 
Mwalimu Mkuu anaishi hapa

Eneo la Shule upande wa Nyuma



                                         
                                              Moja kati  ya Nyumba za Walimu
                                        
Mwalimu Mkuu akimshukuru Mh. Sugu kwa Kutembelea Eneo hilo na Ahadi yake ya Kuwasaidia kukamilisha Nyumba nyingine za Walimu zilizobaki



HATUA YA NNE (UKAGUZI WA DARAJA LILOJENGWA KWA NGUVU YA WANANCHI)

Nia kubwa ni kujua Miundombinu ya Eneo hilo inachangamoto gani ili ziweze kutatuliwa na kufanya shughuli za Wananchi wa eneo hilo kwenda vile inavyopaswa kwenda

                                      
                                         Safari ya Mguu kwa Mguu mapaka Darajani


                                    
                                         Njiani anakutana na moja kati ya wazee maarufu wa Eneo hilo, Mzee Mgulula

                                     
 Baada ya Salamu na Kukumbatian kwa Furaha kumuona Mbunge eneo hilo, Mazungumzo mafupi yanafuata

Mh akipewa Maelezo ya Jinsi gani Daraja hili lililojengwa kwa Nguvu za Wananchi lilivyo    Muhimu kwa Maendeleo ya Kata hiyo
                                 TUKAPATA BAHATI YA KUPITA ENEO LA MAJENGO

Maeneo ya Majengo Jijini Mbeya sehemu amabpo Wanachama wa CHADEMA wanafanya Mazoezi ya Kwaya

Akiwapongeza kwa Wazo la kuanzisha Kwaya Maalum ya Chama.
HATAA YA MWISHO KWA LEO ( ENEO LA  SOKOINE  )
  mahala hapa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wanahitaji Msaada wa Mabati na Vifaa vingine ili kuweza kukamilisha Ujenzi wa Jengo lao



Mh. Sugu aliahidi kuwasaidiaa Vijana hao kukamilisha Jengo hilo ili waweze Kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo.!
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi anaendelea na Ziara katika Kata Mbalimbali ili kukagua Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo na Kuzungumza na Wananchi kwa Kuwapa salam kutoka Bungeni nae Kupewa Salam kutoka katika kila Kata.!!
NJIANI AKIRUDI OFISINI KWA MAJUKUMU MENGINEYO


Alisimama kusalimiana na kila Mmoja na Kujadiliana nae hili na Lile



No comments:

Post a Comment