Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, September 10, 2011

Mh. Joseph Mbilinyi Atoa Pole kwa Watanzania kufuatia kuzama kwa Meli ya Spice huko Zanzibar


Meli ya LCT Spice Islanders ikiwa imezama Pwani ya Nungwi.

Mh. Joseph Mbilinyi ametoa Pole kutokanana na Taarifa za Kuzama kwa Meli ya LCT SPICE ISLANDERS ambayo imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Kwa Taarifa za Awali zinasema kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mh Issa Haji Ussi amethibitisha tukio hilo na kusema ajali  imetokea milango ya saa 8:30 za usiku wa kuamkia leo, na kuongezea kuwa  meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.

Mh Ussi  amesema meli hiyo iliyokuwa imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.

Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Habari hii ni kwa Hisani ya www.wakalinext.blogspot.com

1 comment:

  1. Mheshimiwa hiyo picha a meli ningeomba itolewe sababu inapotosha watanzania. Picha hiyo imechakachuliwa na vyombo vya habari kutoka Meli iliyozama huko Philipines
    Bofya
    http://newsinfo.inquirer.net/tag/trans-asia-shipping-lines-inc
    Nogu

    ReplyDelete