Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Thursday, September 2, 2010

MWANAMUZIKI/MWANAHARAKATI MKOLONI ANYWESHWA SUMU

Mkoloni hapa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari 

Habari zilizotufikia zinaeleza kuwa Mwanamuziki na Mwanaharakati Mkoloni wa kundi la Wagosi wa Kaya ambaye ni mshirika wa karibu sana wa Mr II Sugu katika harakati zote kuanzia za muziki mpaka kwenye jukwaa la siasa, amewekewa sumu katika chakula alichokula katika moda ya Bar kubwa iliyopo eneo la Sinza Dar es salaam.


Habari hizo zimethibitisha kuwa Mkoloni ambaye kwa sasa amelazwa katika moja ya hospitali kubwa jijini alifikwa na balaa hilo alipokwenda kujipatia kifungua kinywa katika Bar hiyo na ndipo alipokutwa na dhahama hiyo ambapo baada ya kuzidiwa alikimbizwa hospitali ambapo anaendelea na matibabu.


Tukio hilo ambalo limeripotiwa polisi limeacha maswali mengi ikizingatia Mwanaharakati huyo siku za hivi karibuni amekuwa mstari wa mbele kutetea haki ya wasanii na yuko mstari wa mbele katika harakati za CHADEMA katika uchaguzi huu na pia yuko bega kwa bega na Mgombea Ubunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi hadi kwenye majukwaa ya kampeni mjini Mbeya.


HABARI KAMILI TUTAWALETEA KARIBUNI.

No comments:

Post a Comment