Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Thursday, September 2, 2010

HISTORIA YA HARAKATI

(Uchambuzi wa Nyimbo za Mr II – SUGU)
Wimbo tunaoupitia leo unaitwa:

NI NDOTO
Mwanamuziki: Mr II - Sugu
Album: Nje ya Bongo
Mwaka: 1999

KIITIKIO:
Ni ndoto, ni ndoto, ni ndoto x 3
(ni ndoto)
Rudia x 4

Ubeti wa 1:
Hautapata rafiki kama mimi mimi ni msema kweli
Ndoto zinaweza kuwa za kweli au zisiwe za kweli
Lazima utazame mbali
Unapoota unapata haina maaana ndio unapata hata
Ni kitu ambacho ni sawa kula kwa macho
Kipi kikusikitishacho
Hakuna ajabu kwa wa kwanza kuwa wa mwisho
Maisha yanaambatana na vitisho
Huyu hatasema hivi kuhusu Yule na Yule atasema vile
kuhusu huyu hapa na pale na hii ni methali ya watu wa kale
Akuanzae mmalize wacha kusema sana
Wacha kuota ndoto za mchana
Kila mtu anaota ndoto maskini anaota ndoto kuwa tajiri
Na tajiri anaota ndoto kuwa tajiri zaidi
Ndipo dhuluma inapozidi
Na watu wengine wanauana inapobidi
Kila mtu anaota pesa yes hata Wanasiasa
Na haswa wanasiasa wa sasa

(Rudia Kiitikio)

Ubeti wa 2:

Chok.. ungefanya nini baba asingepata Ubunge
Ungeweza kukimbiza mbio za Mwenge
Maana una unachowaza cha maana
Sana sana unota ndoto za mchana
Unataka hiki na hiki Adidas mara Nike
Wakati kuangaika hutaki
Tukueleweje salama au walama
Sema kama hauna noma hapa ndiyo Darisalama
Na sisi ndiyo wasanii tunazungumza kisanii
Dizaini hii tuko wachache sana kwenye jamii
Tuna mawazo mazito na hatuamini sana ndoto
Na kama ndoto zote zingekuwa za kweli
Watabiri wangekuwa matajiri najaribu kufikiri
Wangewapata mpaka mawaziri wa serikali
Hakuna binadamu anayetosheka
Maisha yote ni mashaka
Kila mtu hawezi kupata kila kitu anachotaka
Ni ndoto na kucheza na maisha ni sawa kucheza na ndoto
Samahani ningependa kutoa wito
Vijana wavulana na wasichana
Tuendelee kukazana tu usiku na mchana
Hakuna kusema hapana
Daima mbele kurudi nyuma ni mwiko
Chok.. inakubidi ukubali mabadiliko
Usilete zako za 1947 1999
kila mtu anaota ndoto za pesa kisa kutesa
Nani atafanya makosa

(Rudia Kiitikio)

Usiku naota ndoto napigana na shetani
Mchana naota ndoto natoa hotuba bungeni
Mwaka 2000 Rais ni nani
Ni ndoto x 5

MWISHO

Kuanzia kesho tutakuwa tukiuchambua wimbo huu, toa maoni kuhusu mtazamo wako na unadhani msanii dhamira yake ilikuwa ni nini, maoni yako nk.
Uchambuzi utaongozwa na: Kwame Anangisye

1 comment:

  1. INABIDI UPLOAD HUU WIMBO TUUSIKILIZE TENA UMETUTOKA..PLEASE

    ReplyDelete