Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, September 14, 2013

DR. SLAA & MH. JOSEPH MBILINYI - SUGU KUITIKISA MBEYA JUMAPILI HII

NI MKUTANO MKUBWA UTAKAOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE JUMAPILI HII TAREHE 15/9/2013 KUANZIA SAA 8.00 MCHANA
Katibu wa CHADEMA DR. W.P. SLAA

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi - Sugu
 
Mkurugenzi wa Sera, Tafiti na Uratibu wa CHADEMA Mwita M. Waitara
 
Wakazi wa Mbeya na vitongoji vyake wanatarajia kujumuika katika mkutano wa hadhara Utakaofanyika jumapili hii tarehe 15/9/2013 kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja vya Ruanda Nzovwe maarufu kwa siku za karibuni kwa jina la uwanja wa Dr. Slaa. Mkutano huo unaosubiriwa kwa hamu na maelfu ya wakazi wa jiji la Mbeya utahutubiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Willbrod Slaa, Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi na viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mkurugenzi wa Sera, Tafiti na Uratibu wa chama hicho Mwita M. Waitara.
 
Katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo suala la mambo yanayoendelea bungeni na hii itakuwa ni fursa kwa Mbunge wa Mbeya Mjini kukutana na wakazi wa Mbeya waliokuwa wakimsubiri kwa hamu baada ya Mbunge wao kutoka bungeni ambapo kulikuwa na sekeseke lililohusiana na suala hilohilo la katiba.
 
Leo hii jumamosi Viongozi hao wako Chunya Mbeya ambako pia wanahutubia katika mkutano wa hadhara unaofanyika Chunya ambapo program ya CHADEMA ni Msingi inaendelea.


No comments:

Post a Comment