Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Saturday, September 21, 2013

Dr Slaa Awasili Washington DC, Marekani
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipungia mkono baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Dulles nchini Mareani leo tarehe 21 Septemba 2013. Dr Slaa anatarajia kufanya mkutano na Wakazi wa Washington dc tarehe 22 septemba 2013 katika Ukumbi wa Mirage uliopo University BLVD.

Pichani ni makamanda waliojitokeza Uwanja wa Ndege wa Dulles Kumpokea Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ambaye anatarajia kufanya Mkutano na Watanzania wanaoishi Washington DC na maeneo mengine yaliyo karibu.


 

Dr Slaa akipeana Mkono na Katibu wa Tawi na Afisa wa Habari wa Tawi la Chadema Washington DC (DMV) Mh Liberatus Mwang'ombe mara baada ya Dr Slaa kufika Marekani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipeana mkono na Katibu wa Baraza la wanawake Bi Baybe Mgaza uwanja wa ndege wa Dulles alipowasili akitokea Tanzania.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Akipena mkono na Katibu wa Baraza la wazee Mh Elias Mshana uwanja wa ndege wa Dulles Marekani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipeana mkono na Mweka Hazina wa Tawi la Chadema Washington DC (DMV) Mh Ludigo Mhagama kwenye uwanja wa Ndege wa Dulles nchini Marekani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Akiwa na watoto wa Mbunge wa Viti maalum wa Chadema Kwimba Mh Leticia Nyerere, Julia Nyerere (Kushoto) na Helena Nyerere (Kulia).

No comments:

Post a Comment