UZEMBE WA TANESCO WASABABISHA KIFO CHA BINTI WA MIAKA 26 JIONI HII MBALIZI MBEYA.
HAPA
NDIPO MAREHEMU ALIPOGUSA NA KUKUTWA NA MAUTI
NYAYA ZA
UMEME AMBAZO ZIMENING'INIA MITA MOJA KUTOKA USAWA WA ARDHI ZIMESABABISHA KIFO
CHA NEEMA B. KIPENYA (26) ALIPOTELEZA NA KUKAMATA NYAYA HIZO KISHA KUFARIKI PAPO
HAPO.
KATI YA
NGUZO HADI NGUZO NI UMBALI WA ZAIDI YA MITA 75 MAHALI AMBAPO PALIPASWA KUWA NA
NGUZO TATU LAKINI IKAWEKWA NGUZO MOJA , HALI MTEJA WA ENEO HILO ALIKUWA AMELIPIA
NGOZO TATU ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA .
HAPA
NDIPO ALIPO TELEZA MAREHEMU NEEMA NA KUANGUKIA NGUZO HIZO
ASKARI
AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MASHUHUDA
MWENYEKITI
WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO BWANA KISMAN MWANGOMALE AMBAYE NDIYE MTEJA WA KWANZA
KULIPIA TANESCO NGUZO TATU NA KUFUNGWA NGUZO MOJA , NA AMETOA TAARIFA MARA
KADHAA TANESCO NA HATA KUANDIKA BARUA KWA NIABA YA KIJIJI LAKINI HAKUNA
UTEKELEZAJI ULIOFANYIKA HADI MADHARA YAMETOKEA NDIPO TANESCO
WAMEFIKA.
MMOJA
KATI YA WATUMISHI WA TANESCO AMBAYE ALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUKATA UMEME
USILETE MADHARA ENEO HILO , HATA HIVYO ALINUSURIKA KUPIGWA NA WANANCHI WENYE
HASIRA KALI AMBAO WALIKERWA NA TUKIO HILO.
MWENYEKITI
WA KIJIJI CHA MSHIKAMANO WA KWANZA KUSHOTO NA WATUMISHI WA TANESCO WAKIANGALIA
NGUZO ZILIZO ELEMEWA NA UZITO WA NYAYA HIZO NA KUSABABISHA NGUZO KUSHINDWA
KUHIMILI UZITO WA NYAYA HIZO.
WAOMBOLEZAJI
WAKILIA KWA UCHUNGU KWANI MUDA MFUPI ULIOPITA WALIKUWA NA MAREHEMU NYUMBANI
HAPO.
PICHA NA
EZEKIEL KAMANGA
NA MBEYA
YETU BLOG
Chanzo: Mbeya Yetu Blog
No comments:
Post a Comment