Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Tuesday, October 9, 2012

Fuatana na Mbunge SUGU kwenye Mazishi ya Padre Theo John Slaats, Mbeya mjini leo...

Marehemu Padre Theo John Slaats
Wananchi wa Mbeya walifurika kwenye kanisa Katoliki Parokia ya Ruanda, Ilomba - Mbeya Mjini
Jeneza la Padre Slaats katika misa ya mazishi
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro akitoa salamu za rambirambi kanisani
Mh. Joseph Mbilinyi akipita mbele ya kanisa kutoa salamu za rambirambi
 Mh. Sugu akitoa rambirambi zake kwa Askofu Mkuu wa Katoliki jimbo la Mbeya Mhashamu Evarist Chengula
Mbunge akitoa salamu za rambirambi kwa waumini katika misa ya mazishi ya Padre Slaats
 
Mbunge akirudi kuketi baada ya kutoa salamu zake za rambirambi
Mapadre kutoka maeneo mbalimbali nchini walihudhuria mazishi hayo
Askofu Mkuu wa Katoliki jimbo la Mbeya Mhashamu Evarist Chengula akitoka kanisani
Mh. Mbunge akiwa na Mtawa Mkuu wa jimbo la Mbeya katoliki
Mh. SUGU akiwa na Mzee wa kanisa wakati wa mazishi hayo
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akisign kitabu cha maombolezo katika mazishi hayo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro akiongea na Mh. SUGU katika mazishi hayo
Mkuu wa Mkoa Bw. Abbas kandoro akisalimiana na Mama Mbilinyi (Mama mzazi wa Mbunge Sugu) huku Mbunge huyo akiwa katikati
Mh. Mbunge akisalimiana na Askofu Mkuu wa Katoliki jimbo la Mbeya Mhashamu Evarist Chengula
Askofu Mkuu, Mkuu wa Mkoa wakimsikiliza Mbunge
 
Mbunge akiwa eneo la maziko yaliyofanyika katika kanisa hilohilo la Katoliki Parokia ya Ruanda, Ilomba - Mbeya Mjini
Umati wa wananchi wakishuhudia maziko hayo
Mh. Mbunge akiweka shada la maua katika kaburi la Padre Slaats

Askofu Mkuu, Mh. Mbunge na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakitoka eneo la maziko

Monday, October 8, 2012

MH. JOSEPH MBILINYI (SUGU) ALIPOFANYA MKUTANO WA HADHARA UYOLE YA KATI - MBEYA ...

Mh. Mbunge Sugu akiwasili katika eneo la mkutano..
Mbunge Joseph Mbilinyi akiwahutubia wananchi..
Wananchi wa Uyole kati Mbeya wakimsikiliza Mbunge wao
Baadhi ya wananchi wakisikiliza mkutano wa Mbunge wao Joseph Mbilinyi
Mbunge akiagana na wananchi baada ya kumaliza mkutano wake...
Mh. Mbunge alipata fursa ya kula chakula na makamanda wa Uyole - Mbeya
 

Saturday, October 6, 2012

Mh. Mbunge wa Mbeya mjini alipotembelea kituo cha yatima cha Grassroots Tanzania kilichopo Forest-Mpya,Mbeya Mjini...

 ...Mh Mbunge akikaribishwa na meneja wa kituo (katikati) pamoja na Askofu Mwaitolage(kulia) ambaye ndiye anaendesha kituo hiki...
 Meneja akiongea na jambo na Mbunge....
 Mbunge akisalimia watoto....
 Mbunge akizungumza na watoto wa kituo cha Grassroots Tanzania...
 

Thursday, October 4, 2012

TANGAZO

TUMESHAKAMILISHA MCHAKATO WA MFUKO WA ELIMU MBEYA YAANI 'MBEYA EDUCATION TRUST FUND' NA OFISI YETU IKO KATA YA NZOVWE JIJINI MBEYA-KWAHIYO TUNAWAOMBA WANA-MBEYA WOTE PAMOJA NA MARAFIKI WA MAENDELEO YA MBEYA POPOTE MLIPO SASA MUANZE KUTUUNGA MKONO KWA HALI NA MALI ILI TUWEZE KUFANIKISHA MALENGO YA KUPELEKA WATOTO WETU WASIO NA UWEZO SEKONDARI,HIGH SCHOOLS NA VYUO VIKUU...TUMA MCHANGO WAKO KWA MBEYA EDUCATION TRUST FUND A/C NO. 0150421214700-CRDB MWANJELWA BRANCH..TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU KUTOKA MBEYA...

SIKU BONGO MOVIE STAR RAY ALIMPOMTEMBELEA MH. SUGU NYUMBANI KWAKE

 Ray Kigosi kushoto, Mh. SUGU katikati pamoja na Hartman Mbilinyi kulia wakiwa katika picha ya pamoja


MH.SUGU ALIPOONGEA NA WANAWAKE WA BAWACHA - KATA ZA MBEYA

 Hapo akipokelewa na wanawake... alipowasili kwa ajili ya Mkutano huo
 
 Mmoja wa Wanawake akichangia maoni yake kwa Mbunge
 Mh. Joseph Mbilinyi hapo akiwa anaaga baada ya kumaliza mkutano

JINSI AJALI MBAYA YA MAGARI IKILIHUSISHA LORI LA MAFUTA ILIVYOTOKEA MBEYA

 HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO
 MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI
 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
 HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
 HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA 
 FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
 ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU NANE.
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
 HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
 HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI  MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWAALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYO UNGUWA MOTO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO HUO.
 
Mkuu wa mkoa Mbeya Abas Kandoro akiangalia ajali liyotokea mbalizi mbeya mchana wa leo


Watu 8 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa akiwemo Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa baada ya lory  la mafuta kufeli breki wakati likitelemka mlima wa Iwambi Mji wa Mbalizi na kuyagonga magari matatu ambapo kati ya hayo magari mawili yaliteketea kwa moto .
Imeelezwa kuwa ndani ya gari la Mbunge huyo kulikuwepo na watu wawili dereva wa gari hilo aliyejeruhiwa miguuni na kichwani huku   mwanamke mmoja anayesadikiwa kuwa  ni Katibu wa Mbunge huyo ambaye inadaiwa ameteketea  kwa moto na kubaki mifupa na majivu.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nane za mchana katika eneo la  Mteremko wa Iwambia mbapo alisema Lory hilo la mafuta likiwa na namba T81 4BTC na tela lenye namba T815 BT linadaiwa kufeli breki na kuyagonga magari matatu likiwemo gari la Mbunge huyo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro, akizungumza na waandishi kwenye eneo la tukio alisema ajali hiyo imesababishwa na magari manne ambapo kati yao matatu yameteketea kwa moto papo hapo likiwemo gari la Mbunge Toyota  Hilux.
Alisema,  gari lingine lililoteketea moto ni gari ndogo ya abiria Toyota Hiace yenye namba T587 AHT ambalo lilikuwa na watu kumi ambao kati yao wapo waliofariki na kujeruhiwana lory lenyewe la mafuta limeteketea kwa moto.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alisema baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ni Mbunge Mary Mwanjelwa ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Teule ya Ifisi baada ya kuumia kwenye kiuno na dereva wake ambaye ameumia miguu na kupata majeraha kichwani.
Majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi na wengine hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kwamba hali ya Mbunge inaendelea vizuri.
Mtanzania, lilizungumza na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao walisema kuwa Lory hilo la mafuta lilikuwa likishusha mlima huo wa Iwambi, huku mbele yake kulikuwa na Lory lingine la mizigo mbapo dereva wa gari hiyo alifanikiwa kulipisha Lory hilo na ndipo lilipoyagonga magari hayo mawili ambayo mbali na kupinduka kandokando ya barabara pia yaliteketea kwa moto.
“Lory  la mafuta lilikuwa katika mwendokasi na ndipo lilipoligonga lory lingine la mizigo na kisha kwenda kuyagonga magari madogo mawili  na kusababisha ajali hiyo kutokea,”alisema Alisi Mwakisapi.
Alisema, Mbunge wa viti maalumu aliokolewa na bodaboda iliyokuwa karibu na eneo hilo kwa kile alichokidai kuwa mara baada ya kufanikiwa kutoka ndani ya gari hilo dereva huyo alimuona na kumchukua kwenye bodaboda na kumuwahisha hospitali.
“Katika gari alilikuwa amepanda Mbunge, alikuwemo dereva na mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuteketea kwa moto,”alisema

Hata hivyo, miili ya marehemu tisa imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya na hospitali Teule ya Ifisi majina yao hayajatambuliwa na kwamba mwili  wa mwanamke  mmoja  ambaye alikuwa kwenye gari ya Mbunge uliteketea kwa moto.
Chanzo cha habari ni Mbeya Yetu Blog