Msimu wa Ligi Kuu ya soka ya England
umeanza kwa kishindo kwa Aston Villa kuwashtua Arsenal kwa mabao 3-1 katika
uwanja wa Emirates.
Benteke alifunga mabao mawili
Arsenal ndio waliofungua mlango
katika dakika ya 6 kupitia Olivier Giroud. Lakini mabao mawili ya Christian
Benteke kwa mikwaju ya penati yaliwakatisha tamaa mashabiki wa Arsenal.
Bao la tatu la Villa limefungwa na
Antonio Luna.
Wengine walioshinda ugenini ni
Fulham walioifunga Sunderland bao moja kwa bila na Southampton waliilaza West
Bromwich pia kwa bao moja kwa bila liliofungwa na Rickie Lambert. Liverpool
iliibuka na ushindi wa chupu chupu wa bao moja kwa bila dhidi ya Stoke City
liliofungwa na Daniel Sturridge, goli la kwanza kufungwa msimu huu.
Mlinda lango Mignolet aliiokoa
penalti katika dakika za mwisho za mchezo huo. Westham United waliwakaribisha
Cardiff City katika ligi kuu kwa kuwafunga mabao mawili kwa bila. Norwich City
ilitoka sare mawili kwa mawili na Everton.
Source: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment