Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefunga rasmi mikutano yake ya
kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Rasimu ya Katiba mpya kupitia
mabaraza huru ya chama hicho, jijini Dar es Salaam. Chama
hicho kimesema kimefanikiwa kukusanya maoni ya wananchi milioni tano na
kwamba wanatarajia kupeleka maoni hayo kwenye ofisi za Tume kwa lori
kwa kuwa ni mengi.
Akifunga
mikutano hiyo juzi jijini humo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod
Slaa, alisema katika mikutano 49 waliyoifanya ndani ya mikoa tisa
nchini, wamekusanya takribani maoni milioni tano kutoka kwa Watanzania
kuhusu maboresho ya rasimu hiyo dhidi ya milioni mbili yaliyokusanywa na
Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa wanachama wake.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo juzi katika viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, wakati akihitimisha mkutano wake wa mabaraza huru ya kukusanya maoni kwa Watanzania juu ya Rasimu ya Katiba mpya. Alisema, Chadema wanaunga mkono Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, lakini wanapingana naye katika baadhi ya vipengele kama vile Tanzania Bara kuitwa Tanganyika.
Baadhi ya wananchi waliokuwapo kwenye mkutano huo walipendekeza kuongezwa kwa vipengele vya haki kwenye tunu za taifa.Tunu saba za taifa ambazo zimependekezwa katika rasimu hiyo ni utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya taifa.
Wananchi hao walipendekeza kwamba kwenye rasimu hiyo kiongezwe kipengele kinachomruhusu kila Mtanzania kuwa na haki ya kumiliki ardhi, kupata huduma bora za afya kama viongozi wa serikali na wabunge wanavyofanyiwa.
Dk. Slaa alisema katika mikutano hiyo wamezunguka katika mikoa tisa na kufanya mikutano 49 huku zaidi ya Watanzania milioni tano wakiwa wametoa maoni yao juu ya rasimu hiyo.

No comments:
Post a Comment