18 Agosti,
2013 - Saa 19:22 GMT
Magoli 2 yaliyofungwa katika kipindi cha kwanza,moja la Oscar na lingine la
Frank Lampard yameiwezesha Chelsea kufunga Hull.
Kabla ya Chelsea kuliona lango,Lampard alikuwa amekosea mkwaju
wake wa penalty uliopanguliwa na kipa Allan McGregor,lakini muda mfupi baadae
Oscar akanusa nyavu kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Kevin de
Bruyne.
Lampard aliihakikishia Chelsea kuongoza na kuondoka na ushindi kwa kuingiza
bao la pili.
Hull iliyopanda daraja msimu huu, juhudi zake za kujaribu kusawazisha katika
kipindi cha pili hazikufua dafu baada ya walinzi wa Chelsea kuwa makini na
kudhibiti sawa sawa nafasi zao.
Kwa ushindi huo wa kwanza wa Mourinho tangu aliporudi kuifundisha tena
Chelsea,meneja huyo sasa anaweza kuelekeza macho yake na mbinu zake kwa mechi
itakayofwatia ,Chelsea itakapoikaribisha Aston Villa jumatano.
Mapema ya hapo,Tottenham walijipatia ushindi wa goli 1 bila kwenye uwanja wa
Crystal Palace kupitia mshambuliaji wao mpya Roberto Soldado aliyetikisa nyavu
kunako dakika ya 50 kwa njia ya penalty.
No comments:
Post a Comment