Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Wednesday, August 21, 2013

SUGU ATUA JIMBONI: Asisitiza wananchi kujitokeza kwenye mkutano unaohusu katiba mpya.

Mh. Joseph Mbilinyi - Sugu, moja ya picha akiongea na wakazi wa Mbeya 

Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi amerejea jijini Mbeya baada ya kutokuwepo jimboni kwa takribani wiki mbili na nusu, Mbunge huyo alikuwa nje ya Mbeya kwa ajili ya shughuli za Kamati ya Bunge pamoja na shughuli nyingine mbalimbali zikiwemo ziara katika mikoa mbalimbali.
 
Kwa mujibu wa Mbunge huyo anasema amerejea jijini Mbeya kwa siku kadhaa kwa lengo la kuchukua maoni mbalimbali ya Wananchi kama ilivyo ada yake kabla ya kwenda kuhudhuria kikao cha Bunge wiki ijayo.
 
Joseph Mbilinyi pia amewahimiza wananchi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika zoezi la ukusanyaji maoni juu ya katiba mpya, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali.
 
Sugu pia alisisitiza wananchi wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla kuunga mkono msimamo wa CHADEMA kuhusu maoni ya katiba mpya, haswa mambo muhimu kama vile kumpuguzia Rais madaraka na hoja ya Tanzania kuwa na serikali tatu.
 
Wakati huohuo Mbunge huyo amewataka wakazi  Mbeya  kujitokeza kwa wingi katika Mkutano utakaofanyika  Alhamisi tarehe 22/8/2013 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe ambao utaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho ambao ni mfululizo wa ziara inayofanyika nchi nzima ikiongozwa na Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA  kuhusiana na rasimu ya mabadiliko ya katiba.
 
 

No comments:

Post a Comment