Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Wednesday, January 11, 2012

DKT SLAA NA MH SUGU WAFANYA MKUTANO MKUBWA KATA YA NZOVWE JIJINI MBEYA

Dkt Slaa akijadiliana jambo na katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya katika mkutamo kata ya Nzovwe jijini Mbeya

Mh sugu akiwahutubia wakazi wa Nzovwe kabla haja mkaribisha Dkt Slaa jukwaani

Joseph Mbilinyi (Sugu) akiwaelezea Wanambeya  mchanganuo wa mfuko wa elimu jimbo la Mbeya mjini,na kufanya wakazi wa Nzovwe kuonyesha kuguswa sana na mpango huu wa elimu utakao nyanyua matumaini makubwa kwa vijana wa Mbeya mjini kwa kupata fursa za kulipiwa ada za vyuo vikuu kwa watakao fanya vizuri na wasio jiweza.
Dkt  Slaa akiwashukuru wakazi wa Nzovwe kwa kukiamini Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika uchaguzi mdogo kwa kumchagua Diwani kutoka CHADEMA. 

Umati mkubwa wa wanambeya ukimshamgilia kwa furaha kubwa Dkt Slaa wakati akiwahutubia
Baada ya mkutano maelfu ya Wanambeya wakawasindikiza Slaa na Sugu mpaka hotelini kwa maandamano takriban kilomita tano kutoka viwanja vya mkutano

Dokta akisisitiza jambo kwa mwenyeji wake Mh Sugu
''.......Chademaa chama makini ....Chademaa mkombozi wetu .....''. Wanambeya wakiimba kawa furaha kubwa

Mh Sugu na Dkt Slaa wakiwapungia mikono wakazi wa stendi kuu wakati wakipita kwa maandamano makubwa ya amani ya kipekee kabisa kuwahi tokea jijini Mbeya

No comments:

Post a Comment