Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Thursday, October 4, 2012

JINSI AJALI MBAYA YA MAGARI IKILIHUSISHA LORI LA MAFUTA ILIVYOTOKEA MBEYA

 HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO
 MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI
 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
 HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
 HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA 
 FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
 ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU NANE.
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
 HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
 HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI  MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWAALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYO UNGUWA MOTO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO HUO.
 
Mkuu wa mkoa Mbeya Abas Kandoro akiangalia ajali liyotokea mbalizi mbeya mchana wa leo


Watu 8 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa akiwemo Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa baada ya lory  la mafuta kufeli breki wakati likitelemka mlima wa Iwambi Mji wa Mbalizi na kuyagonga magari matatu ambapo kati ya hayo magari mawili yaliteketea kwa moto .
Imeelezwa kuwa ndani ya gari la Mbunge huyo kulikuwepo na watu wawili dereva wa gari hilo aliyejeruhiwa miguuni na kichwani huku   mwanamke mmoja anayesadikiwa kuwa  ni Katibu wa Mbunge huyo ambaye inadaiwa ameteketea  kwa moto na kubaki mifupa na majivu.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nane za mchana katika eneo la  Mteremko wa Iwambia mbapo alisema Lory hilo la mafuta likiwa na namba T81 4BTC na tela lenye namba T815 BT linadaiwa kufeli breki na kuyagonga magari matatu likiwemo gari la Mbunge huyo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro, akizungumza na waandishi kwenye eneo la tukio alisema ajali hiyo imesababishwa na magari manne ambapo kati yao matatu yameteketea kwa moto papo hapo likiwemo gari la Mbunge Toyota  Hilux.
Alisema,  gari lingine lililoteketea moto ni gari ndogo ya abiria Toyota Hiace yenye namba T587 AHT ambalo lilikuwa na watu kumi ambao kati yao wapo waliofariki na kujeruhiwana lory lenyewe la mafuta limeteketea kwa moto.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alisema baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ni Mbunge Mary Mwanjelwa ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Teule ya Ifisi baada ya kuumia kwenye kiuno na dereva wake ambaye ameumia miguu na kupata majeraha kichwani.
Majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi na wengine hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kwamba hali ya Mbunge inaendelea vizuri.
Mtanzania, lilizungumza na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao walisema kuwa Lory hilo la mafuta lilikuwa likishusha mlima huo wa Iwambi, huku mbele yake kulikuwa na Lory lingine la mizigo mbapo dereva wa gari hiyo alifanikiwa kulipisha Lory hilo na ndipo lilipoyagonga magari hayo mawili ambayo mbali na kupinduka kandokando ya barabara pia yaliteketea kwa moto.
“Lory  la mafuta lilikuwa katika mwendokasi na ndipo lilipoligonga lory lingine la mizigo na kisha kwenda kuyagonga magari madogo mawili  na kusababisha ajali hiyo kutokea,”alisema Alisi Mwakisapi.
Alisema, Mbunge wa viti maalumu aliokolewa na bodaboda iliyokuwa karibu na eneo hilo kwa kile alichokidai kuwa mara baada ya kufanikiwa kutoka ndani ya gari hilo dereva huyo alimuona na kumchukua kwenye bodaboda na kumuwahisha hospitali.
“Katika gari alilikuwa amepanda Mbunge, alikuwemo dereva na mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuteketea kwa moto,”alisema

Hata hivyo, miili ya marehemu tisa imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya na hospitali Teule ya Ifisi majina yao hayajatambuliwa na kwamba mwili  wa mwanamke  mmoja  ambaye alikuwa kwenye gari ya Mbunge uliteketea kwa moto.
Chanzo cha habari ni Mbeya Yetu Blog

No comments:

Post a Comment