Wednesday, July 16, 2014
Monday, July 14, 2014
Chadema Blog: TANZANIA NAMNA HII, MALIASILI NA UTALII UKO SHAKAN...
Chadema Blog: TANZANIA NAMNA HII, MALIASILI NA UTALII UKO SHAKAN...: Hii ndiyo video ambayo Mheshimiwa Peter Msigwa (MB), Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, aliiwasilisha ndani ya bunge kama sehemu ya ushah...
Sunday, July 13, 2014
ZIARA ZA MBUNGE JOSEPH MBILINYI JIMBONI: HAPA NI ISYESYE - MBEYA
Saturday, July 12, 2014
MBUNGE SUGU: AKABIDHI KAZI YA UJENZI WA DARAJA LA IYELA(MAKABURINI)
Mbunge wa
Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" amekabidhi kazi ya ujenzi wa
daraja la Iyela(makaburini) kwa mkandarasi na tayari ujenzi huo umekwisha anza,
daraja hilo kwa mujibu ya maelezo litajengwa
likiwa limenyanyuliwa sana juu na litakuwa likipitisha magari yenye uzito hadi tani 10, na pichani ni kivuko ambacho kilianza kujengwa
miaka zaidi ya 25 iliyopita na hakikukamilika.
Kwa
wakazi wa Mbeya daraja hilo ni muhimu sababu ndiyo wanaitumia wananchi wa Mbeya
kwa shughuli zao mbalimbali na haswa maziko sababu ndiyo eneo lina makaburi
yanayotumiwa sana na wakazi wa Mbeya kwa maziko, na tatizo la daraja hilo
lilipelekea watu kuzunguka umbali mrefu ili kufikia eneo hilo.
Friday, July 11, 2014
Thursday, July 10, 2014
SUGU AJIBU MAPIGO YA CCM

BAADA
ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kumshambulia Mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), ukimuita mpangaji katika jimbo hilo,
amewajibu akisema kuwa wanaota ndoto za mchana.
Mbilinyi
maarufu kama Sugu, alisema vijana hao hawazijui siasa za jimbo hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa jana, Sugu, alisema vijana hao
ndio wapangaji, na kwamba wasitarajie mteremko kwani yeyote atakayesimamishwa
katika jimbo hilo kupitia CHADEMA ataibuka mshindi kutokana na wananchi wa
Mbeya kuendelea kuwa na imani na chama hicho.
Alisema
jimbo hilo alilikuta kama nyumba mbovu, akaamua kuinunua na baadaye akaivunja
na kupandisha ghorofa, halafu aliyemuuzia anarudi na kudai nyumba ni ya kwake.
“Ndugu
zangu, Jimbo la Mbeya ni sawa na Mkinga ama Mpemba aliyeenda Kariakoo, amenunua
nyumba chakavu akaibomoa na kupandisha ghorofa zaidi ya tatu, halafu aliyeuza
nyumba hiyo anaibuka na kusema hao watu ni wapangaji, si atakuwa anachekesha?”
alihoji.
Aliongeza
kuwa CCM hawana chao katika jimbo hilo kwa sababu sasa CHADEMA wanawaza
kuchukua Halmashauri ya Jiji, na kwamba suala la ubunge haliwapi shida tena.
“Mikakati
yetu ni kuchuka kata zote, lakini ili kuleta changamoto katika baraza ni vema
tukawaachia kata kama nane ili kuleta changamoto katika Baraza la Madiwani,”
alisema.
Kwa
mujibu wa mbunge huyo, viongozi hao wa UVCCM wanafanya mikutano hiyo bila kuwa
na taarifa kamili za jimbo hilo, kwamba ndio maana wamekuwa wakikurupuka na
kutoa shutuma zisizo na ukweli wala utafiti wowote.
Alisema
kuwa katika Kata ya Igawilo kulikuwa na mpango wa kujenga bwawa la samaki,
lakini diwani wa kata hiyo kupitia CCM aliwashawishi viongozi wa serikali
kugomea mradi huo kwa madai kuwa hitaji lao ni madawati.
Sugu
alisema kuwa utafiti alioufanya alibaini mradi huo uligomewa na viongozi wa
serikali za mitaa, ambao walipata shinikizo kutoka kwa diwani.
“Unajua
watu wanaongea sana, ohoo aliahidi kuwa ataleta mradi wa samaki na mpaka sasa
hakuna kitu, wananchi wengi hawajui, utekelezaji ulishaanza, lakini kutokana na
ukiritimba wa baadhi ya wanasiasa pamoja na watumishi wa serikali
wameukwamisha.
“Pale
Uyole Nsalaga tulishachimba bwawa la samaki muda mrefu na nilishaongea na
Mkurugenzi wa Jiji tukabaini kuwa maji yanayohitajika katika bili yake ni kama
sh 200,000 kwa mwezi, lakini mpaka sasa hakuna kitu, wanazungusha tu bila kutoa
sababu za msingi,” alisema Sugu.
Katika
mikutano mingi ya CCM, wamekuwa wakijinadi kuwa jimbo hilo limepangishwa kwa
muda kwa CHADEMA, hivyo uchaguzi ujao watalirejesha bila ugumu wowote.
Wakiongozwa
na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
sherehe za kuwaapisha makamanda wa UVCCM kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Ruanda Nzovwe mwishoni mwa wiki, vijana hao wa CCM walisema kuwa Sugu ni
mpangaji katika jimbo hilo, hivyo ajiandae kuondoka katika uchaguzi ujao.
Wednesday, July 9, 2014
WAANDAMANA KUDAI KIDATO CHA TANO
- WATINGA OFISI ZA MBUNGE JOSEPH MBILINYI NA MKUU WA MKOA
- WAANDISHI WA HABARI NAO WATINGA KUJUA HATIMA YA SAKATA HILI
- SUGU AONGEA NA WAZIRI NA KUHAKIKISHIWA SUALA HILI LITATATULIWA MAPEMA
-
Wahitimu 39 wa kidato cha nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana waliandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa na pia wakaenda kwa Mbunge wa Mbeya Mjini ili kujua hatma yao baada Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kuwapangia nafasi za kujiunga kidato cha tano licha ya kufanya vizuri katika mitihani yao.Wakizungumza wanafunzi na wazazi wao, walisema kuwa waliamua kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa pamoja na Mbunge wa Joseph Mbilinyi - Sugu ili kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi majibu ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wa chini yake.Walisema tangu wizara itangaze majina kwa ajili ya kujiunga kidato cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa kuona wanafunzi kutoka shule hiyo hawajapangiwa kwa ajili ya kuendelea na masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa na ufaulu mzuri.Wanafunzi hao ambao wamepata alama za daraja la kwanza hadi tatu, hawajui hatima yao kutokana na wizara husika kushindwa kuwapangia shule kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.Nao wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa, hakuna majina ya watoto wao na hatima ya watoto wao kwa sasa iko chini ya Mbunge wao huyo ili awasaidie kutatua hili suala.Mbunge huyo wa Mbeya mjini aliweza kuongea na Naibu Waziri wa Tamisemi - Elimu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri huyo kumuhakikishia kuwa tatizo hilo lililotokana na Baraza la mitihani kutofikisha majina ya wanafunzi hao wizarani kwa wakati lakini limeshafika mezani kwake hivyo atahakikisha linatatatuliwa ndani ya siku chache zijazo.Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika shule hiyo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa ajili ya kuendelea na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa alama nzuri.
Subscribe to:
Posts (Atom)














































