Wahitimu 39 wa kidato cha nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari
Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana waliandamana hadi ofisi za Mkuu
wa Mkoa na pia wakaenda kwa Mbunge wa Mbeya Mjini ili kujua hatma yao baada
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kuwapangia nafasi za kujiunga
kidato cha tano licha ya kufanya vizuri katika mitihani yao.
Wakizungumza wanafunzi na wazazi wao, walisema kuwa waliamua
kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa pamoja na
Mbunge wa Joseph Mbilinyi - Sugu ili
kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi majibu ya kuridhisha kutoka kwa
viongozi wa chini yake.
Walisema tangu wizara itangaze majina kwa ajili ya kujiunga kidato
cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa kuona wanafunzi kutoka shule hiyo
hawajapangiwa kwa ajili ya kuendelea na masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa
na ufaulu mzuri.
Wanafunzi hao ambao wamepata alama za daraja la kwanza hadi tatu,
hawajui hatima yao kutokana na wizara husika kushindwa kuwapangia shule kwa
ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Nao wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
(CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu kwa
ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa, hakuna majina ya watoto wao na
hatima ya watoto wao kwa sasa iko chini ya Mbunge wao huyo ili awasaidie
kutatua hili suala.
Mbunge huyo wa Mbeya mjini aliweza kuongea na
Naibu Waziri wa Tamisemi - Elimu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri huyo kumuhakikishia kuwa tatizo hilo lililotokana
na Baraza la mitihani kutofikisha majina ya wanafunzi hao wizarani kwa wakati lakini
limeshafika mezani kwake hivyo atahakikisha linatatatuliwa ndani ya siku chache
zijazo.
Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia
kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika shule hiyo
hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa ajili ya kuendelea na
kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa alama nzuri.
No comments:
Post a Comment