Wednesday, May 11, 2011
Mama wa mtoto mwenye matatizo ya kutokuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa akipokea msaada wa Tshs 600,000/= kutoka kwa Mh Joseph O Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini ili aweze kumpeleka Hospitali ya Peramiho kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kwa mujibu wa gharama hiyo ambayo Mama huyo alielezwa ikipatikana ndio ataweza kufanyiwa upasuaji. Mungu atamsaidia atapona!
Mama wa mtoto mwenye matatizo ya kutokuwa na haja kubwa akitoa maelezo ya mtoto wake mwenye umri wa miaka 2 kwa waandishi wa habari na Mh Mbunge wa Mbeya mjini ambaye aliguswa na tatizo la mtoto huyo na kuamua kumsaidia..
Mh Mbunge wa Mbeya mjini akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa NIMR na baadhi ya maafisa waandamizi wa kituo hiko alipotembelea katika moja ya shughuli zake anazozifanya jimboni kwake.
Mh Joseph O Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini akiwa katika moja ya zira anazoendelea kuzifanya na hapa akiwa katika uwanja unaoendelea kujengwa wa Songwe International Airport uliopo Songwe-Mbeya. Katika picha anaonekana akipewa maelezo na Meneja mradi huku wakiwa wamesimama eneo la runaway ambalo tayari km 2 zimewekwa lami na ujenzi bado unaendelea......kwa maelezo ya meneja mradi kufikia mwezi wa 8 tayari uwanja utakuwa umekamilika na kazi inayobaki ni kwa serikali kukamilisha taratibu za ofisi na mambo mengineyo.
Mh Joseph O Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini akiwa katika ziara ya kituo cha utafiti cha NIMR kilichopo Mbeya mjini ndani ya Hospitali ya rufaa,kama anavyoonekana akipata maelezo kutoka kwa Managing dector wa MMRP Mr Leonard Maboko. Baada ya hapo alitembelea maabara zote zilizopo kituoni hapo na kujionea shughuli za utafiti pamoja na kupata maelezo ya kina kuhusiana na shughuli zinazofanywa na kituo hiko
Mh Joseph O Mbilinyi{MP} akiwa katika moja ya ziara zake jimboni Mbeya,hapa alikuwa ametembelea MBEYA DRY PORT na kujionea mazingira yake pamoja na kujadiliana na uongozi kujua ni kwa nini kituo hakifanyi kazi kwani ni moja kati ya sehemu ambayo ingeweza kutoa ajira zaidi ya 300. Kulia ni mkurugenzi wa kituo hiko na kushoto kwa Mbunge ni Fuel Depot manager Mr Suleiman Issa Soloka,akifuatiwa na Mrs Tabu Kaihula......hapa wakiangalia na kuteta jambo juu ya crane ya kunyanyulia containers.
Mkutano uliofanyika Uyole-Kibonde nyasi,Mh Joseph O Mbilinyi akiwashukuru wananchi na pia kuwafafanulia baadhi ya mambo jimboni kwake...hiii ni baada ya kutoka bungeni Dodoma.
Friday, May 6, 2011
CHADEMA WAMSHAMBULIA PROF. MWANDOSYA
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr II Sugu, amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya, kutumia muda wake wa uongozi uliosalia kwa ajili ya kujiandaa na kustaafu kwa kuwa ndoto zake za kutaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haziwezi kutimia.
Pia alisema ni vigumu tena kwake kuendelea kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki.
Sugu aliyasema hayo wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa ‘Chadema Twanga Kotekote’ ulofanyika katika kijiji cha Kandete, eneo la Mwakaleli Jimbo la Rungwe Mashariki ambalo hivi sasa linashikiliwa na Prof. Mwandosya.
Mkutano huo ni moja ya mikutano mingi itakayoendelea kufanyika katika jimbo hilo, ambayo imepewa jina la ‘Operesheni Giant Ndosya, yenye lengo la maandalizi ya kumg’oa Prof. Mwandosya katika jimbo hilo kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Sugu alisema Prof. Mwandosya hajalitendea haki jimbo lake kwa kuwa wananchi hao wamempa ridhaa ya kuwaongoza kwa zaidi ya miaka 15, tena akiwa na wadhifa mkubwa serikalini, lakini kwa muda wote huo ameshindwa kuwajengea wananchi wake barabara kuanzia Katumba hadi Mwakaleli yenye urefu wa kilometa 30 tu.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Joseph Mbilinyi (SUGU) akiwa jukwaani kwenye moja ya mikutano
Alisema hata kama Prof. Mwandosya akichaguliwa kuwa rais hatawakumbuka wananchi wa Rungwe na badala yake atafanyia sherehe za kujipongeza Dar es Salaam, kwa kuwa huku kwao hakuna barabara alizojenga anazoweza kupitisha magari ya Ikulu.
Aidha Sugu alisema anamshangaa Prof. Mandosya kutotumia elimu kubwa aliyonayo kusoma alama za nyakati na kuendeleza fikra za kutaka urais akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho Sugu alidai kuwa kuna kila dalili kwamba kufikia mwaka 2015 chama hicho kinaweza kisiwepo.
“Nawaomba siku akija hapa mpeni ujumbe huu kuwa ajiandae kustaafu kwa kuwa hakuna urais wala ubunge tena kwake, namshauri arudi kufundisha darasani kwa kuwa hilo ndilo bado tunalihitaji kutoka kwake,” alisema Sugu huku akishangiliwa.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala, alisema mikutano ya Twanga Kotekote wilayani Rungwe ambayo imeongezewa jina la ‘Operesheni Giant Ndosya’ inalenga kung’oa meno ya Mwandosya ya utawala wake wa kiimla katika Jimbo la Rungwe Mashariki.
Mwamalala alisema Mwandosya amewalemaza wakazi wa Rungwe Mashariki kimaendeleo na kuwa katika hilo hawawezi kumwonea huruma, hivyo akawataka wananchi wa Rungwe Mashariki kuunga mkono harakati hizo za ukombozi wao.
“Hakuna kumwonea huruma Mwandosya kwa kuwa ametulemaza kimaendeleo, hata hawa madiwani wabovu mliowachagua mmewachagua kwa jina la Mwandosya, kubwa tunalowaombeni wananchi wa Rungwe ni kutuunga mkono katika harakati hizi za ukombozi wa jimbo hili,” alisema Mwamalala.
Kiongozi wa kikosikazi cha Chadema Twanga Kotekote, John Mwambigija, alisema Mwandosya badala ya kufikiria maendeleo ya jimbo lake ameanza kampeni chafu ya kuwarubuni na kuwanunua viongozi wa Chadema na kuwaingiza CCM.
Alidai kuwa kwa kitendo hicho cha Mwandosya ajue kuwa jimboni kwake hayuko salama. Alisema Mwandosya asahau tena ubunge mwaka 2015 na kama anahitaji kupona akimbilie kugombea urais.
Timu hiyo ya Kikosikazi Chadema Twanga kotekote leo inahamia mjini Tukuyu katika jimbo linaloongozwa na aliyekuwa Waziri wa Afya, Prof. David Mwakyusa, kwa ajili ya kuendeleza harakati zake za kukijenga chama.
Baada ya mkutano huo, Chadema Twanga Kotekote itasitisha mikutano yake ili kupisha maandalizi ya maandamano ya kitaifa ya Operesheni Sangara ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 4, mwaka huu jijini Mbeya.
Saturday, April 9, 2011
Studio ya JK yazua mjadala bungeni
| ||
|
Wednesday, April 6, 2011
Mbunge Joseph Mbilinyi apinga kiwanda kugeuzwa ghala la bia.
Na Joachim
Nyambo,Mbeya
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr II, amesema
kitendo cha serikali mkoani hapa kukabidhi majengo ya kilichokuwa
kiwanda cha zana za kilimo (ZZK) yaliyopo eneo la Iyunga jijini hapa
kwa kampuni ya vinywaji ya TBL yatumike kama maghala kinakinzana na
mpango wa serikali wa kufufua viwanda muhimu kama hicho.
Mhe. Joseph Mbilinyi (Sugu) akiwa katika moja ya mikutano yake
Kabla ya kusimamisha uzalishaji wa zana zaidi ya miaka kumi iliyopita
hali iliyosababishwa na mwekezaji aliyekabidhiwa kushindwa kukiendesha
kiwanda hicho kilikuwa tegemeo kubwa la wananchi wa mkoa wa Mbeya
ambao asilimia yao kubwea ni wakulima.
Akizungumza na mamia ya wakazi wa kata za Nsalaga na Uyole katika
viwanja vya kibonde Nyasi, Mbunge huyo amesema hatua hiyo moja kwa
moja imewapa hofu wananchi kuwa huenda serikali haina mpango tena wa
kukifufua ili kiendelee na uzalishaji wa zana hizo ambao utaweza
kuwapunguzuia gharama za ununuzi wa pembejeo tofauti na ilivyo hivi
sasa.
Amesema inashangaza kuona kuwa baadhi ya watendaji wa serikali ambayo
kila siku inahubiri mpango wa kukuza uchumi wa wananchi wake kupitia
kilimo kwa sera mbalimbali ikiwemo Kilimo Kwanza wanakubali kumpa
mwekezaji ambaye anayegeuza kiwanda cha ZZK kuwa ghala la kuhifadhia
bia.
Amesema wananchi wa mkoa wa Mbeya kwa ujumla walikitegemea sana
kiwanda hicho kiweze kufufuliwa na kuzalisha zana za kilimo ambazo
zingepatikana kwa urahisi kwani zingeuzwa kwa bei ndogo kwa wakulima
ili waweze kuboresha kilimo chao lakini sasa matumaini yao yameanza
kufifia.
Mbilinyi amesema kama kiwanda hicho kingefufuliwa hata Trekta ndogo
aina ya Powertiller zinazoagizwa nje ya nchi kwa bei kubwa zingeweza
kuzalishwa katika kiwanda hicho na kuuzwa kwa bei ambayo wakulima
wangemudu kununua.
Hata hivyo Mbilinyi amesema yupo tayari kubisha hodi katika ofizi za
Waziri wa Viwanda ili apewe maelezo ya kina juu ya mwongozo uliotumika
kwa serikali kugeuza kiwanda hicho kuwa ghala la kuhifadhia bia badala
ya kuweka mikakati ya kukifufua.
Aidha Mbunge huyo amepongeza hatua ya seriakali kujenga uwanja wa
ndege wa Songwe , akisema ameridhishwa hatua za ujenzi zinazoendelea
baada ya kuutembelea na kuelezwa na wataalamu kuwa ifikapo Agosti
mwaka huu ndege zitakuwa zimeanza kutua katika uwanja huo.
Mbilinyi amesema kukamilika kwa uwanja huo ni changamoto kubwa ya
maendeleo katika mkoa wa Mbeya na kuwataka wananchi kujiandaa vyema
kuutumia uwanja huo kwa manufaa hususani kwa kuzalisha mazao
yanayoweza kusafirishwa nje ya nchi na kuuzwa kwa bei yenye kuwaletea
tija.
Siku Mhe. Joseph Mbilinyi Alipotembelea Jukwaa La Sanaa
Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kwa Jina la Sugu akiongea na wadau wa Jukwaa la Sanaa jana wakati alipohudhuria kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa mbunge. Sugu ni moja ya wadau wa Jukwaa hilo linalofanyika kila Jumatatu Ukumbi wa BASATA.Profesa Amandina Lihamba kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichokoza mada kuhusu tasnia ya Filamu hapa nchini kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA jana. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego.
Na Mwandishi Wetu:
Jukwaa la Sanaa BASATA limempongeza kwa ushindi wa ubunge na kumpa kazi ya kutetea maslahi ya wasanii Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni mmoja wa waasisi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina Sugu.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye ukumbi wa BASATA kwa niaba ya wadau wote. Profesa Amandina Lihamba kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye alikuwa ni Mratibu wa Jukwaa hilo alisema kwamba, wadau wa Jukwaa la Sanaa wanampongeza kwa dhati kwa ushindi wake na wanamtuma bungeni kutetea haki zao na kwamba asiwatupe.
“Tunajua toka ushinde leo ni mara yako ya kwanza kuonana na hadhira ya wasanii hivyo tunachukua fursa hii kukupongeza kwa dhati, uendelee na moyo huo huo wa kuwapigania wasanii na usiwatupe” aliongeza Profesa Lihamba.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema kwamba, pamoja na BASATA awali kutuma barua ya pongezi kwake na kwa wabunge wengine wasanii, bado Jukwaa la Sanaa lina kila sababu ya kumpongeza na kumtuma kwenda kutetea haki za wasanii na kuhakikisha maslahi ya sekta ya sanaa yanalindwa.
“Naomba niungane na wenzangu kutambua uwepo wa Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, msanii mwenzetu naimani sasa tunapozungumza hapa katika Jukwaa tunazungumza na mtu ambaye sasa atakuwa bungeni akiwakilisha wasanii. Pamoja na barua ya kumpongeza tuliyomtumia yeye na wasanii wengine walioingia bungeni, tunampongeza tena kwa dhati” alisema Materego.
Naye Mbilinyi aliyeambatana na Katibu wake Fred Maliki, maarufu kwa jina la usanii la Mkoloni alimshukuru Materego kwa pongezi zake lakini akapongeza juhudi anazochukua katika kuwahabarisha na kuwapa fursa ya elimu wadau wa sanaa. Aliahidi kuendeleza harakati za kupigania haki za wasanii kwani ndicho kitu ambacho ataanza nacho.
“Harakati za kupigania haki za wasanii nimezianza kwa muda mrefu nawaahidi kwamba sitarudi nyuma na kwa sasa napenda niwaambie kwamba, mapambano ndiyo kwanza yameanza kwani sasa ndiyo tumekabidhiwa rungu” alimalizia Mbilinyi ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama za Mikononi mwa polisi, Deiwaka, Dar moto chini, Wananiita Sugu, Hold On na nyingine nyingi.

Mr II ajisifu kwa kuweka historia bungeni
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr II au Sugu’ ametamba na kujifafanisha na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika kuweka historia ya yeye kuwa msanii wa kwanza wa muziki wa bongo flava kuingia bungeni kama ilivyo kwa Spika ambaye ni mwanamke wa kwanza kuongoza Bunge.
Mbilinyi, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa majigambo hayo jana wakati akisoma maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Azimio la Serikali la Kuridhia Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) la Kulinda Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa mwaka 2003.
Azimio hilo liliwasilishwa jana bungeni na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi. Kabla ya kutoa maoni hayo, Mbilinyi alisema, “Kwa heshima kubwa niwashukuru wananchi wa Mbeya Mjini kuniwezesha kuweka historia ya kuwa msanii wa kwanza wa Bongo Flava kuchaguliwa kuwa Mbunge, Mheshimiwa Spika, mimi na wewe tumeingia katika historia kupitia Bunge hili la kumi, kwa mimi kuwa msanii wa kwanza wa Bongo Flava kuingia bungeni na wewe kuwa Spika wa kwanza mwanamke kuliongoza Bunge,” alisema Mbilinyi na kufanya wabunge kuangua kicheko.
Mbilinyi baada ya kueleza kuwa suala hilo ni la kihistoria na yeye anafarijika ameingia katika historia, alimpongeza Makinda na kuendelea kutoa maoni ya kambi ya upinzani yaliyounga mkono hoja hiyo na kueleza kuwa azimio linalenga kulinda hadhi ya Mtanzania.
Baada ya maoni ya Kambi hiyo ya Upinzani, baadhi ya Wabunge walipata fursa ya kuchangia azimio akiwemo msanii mwingine, Mbunge wa Viti Maalum, Vick Kamata (CCM) ambaye aliunga mkono hoja na kueleza kuwa mkataba huo ukiridhiwa utawawezesha wasanii kutambulika kimataifa na kazi zao kuweza kulindwa kwa kuwa suala la hatimiliki limezingatiwa kwa upana katika mkataba huo.

Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II akipongezwa na Spika wa Bunge Mh Anna Makinda

Naye Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM) alisema kilio cha wasanii wa nyimbo za asili zinazobeba utamaduni wa Kitanzania, kimefika mahali pake na kutaka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, kupigwe nyimbo za asili za makabila yetu badala ya nyimbo za kigeni zinazopigwa hivi sasa.
Monday, March 28, 2011
Saturday, March 12, 2011
mkutano wa kujadili maendeleo Uyole-kibonde nyasi
Mh Joseph O Mbilinyi mbunge wa Mbeya mjini akiwahutubia wananchi wa jimbo la Mbeya mjini katika eneo la Kibonde nyasi Uyole jijini Mbeya pamoja na kuwashukuru pia alikuwa akitumia fursa hiyo kuchukua maswali mbali mbali kwa wananchi kabla ya kwenda Bungeni tarehe 5-4-2011.
Thursday, December 30, 2010
SUGU NA MAISHA YA KILA SIKU KAMA MBUNGE
Mh SUGU akifanya kazi ofisini kwa kwake
Bwana Daniel Kamili ( Danny Msimamo ) akiwa katika meza ya mapokezi tayari kwa kuwa hudumia Wanambeya
Katibu wa Mbunge ( Mkoloni ) pamoja na Sugu nyumbani wakibadilishana mawili matatu mara baada ya kutoka ofisini
Hapa Danny msimamo akibadilishana mawili matatu na Mh SUGU
Sugu akiwa nyumbani kwake
HATIMAYE SUGU AFANYA MKUTANO WAKUWA SHUKURU WANAMBEYA
WanaMbeya waki sikiliza kwa makini hatuba ya Mh Joseph Mbilinyi
Mwenye suti nyeusi ni katibu wa mbunge bwana Fredrik Maliki ( Mkoloni ) akiwa pamoja na Daniel Kamili ( Danny Msimamo )
Akiwasalimia wakazi wajiji la Mbeya
Umati mkubwa ulifurika katika viwanya vya Sido kumsikiliza Mh Mbunge
Mh akisisitiza jambo wakatiakiwa hutubia wananchi wa Mbeya
Thursday, December 23, 2010
TANGAZO LA MKUTANO WA KUWA SHUKURU WANANCHI WA JIJI LA MBEYA
Mh JOSEPH MBILINYI " Leo Ijumaa tarehe 24 Dec,kutakuwa na mkutano wa kuwashukuru wapiga kura,pamoja na kuwatakia Xmas njema wananchi wa Mbeya..Mkutano utafanyika kwenye uwanja wa soko la Sido,Mwanjelwa...Wote mnakaribishwa kwenye mkutano huu wa kwanza wa hadhara toka tushinde uchaguzi...One luv as alwayz!! "
Monday, November 15, 2010
Mh JOSEPH MBILINYI AKIAPA KUWA TUMIKIA WATANZANIA
Mh JOSEPH MBILINYI akiapa kuwa tumikia watanzania na haswa wananchi wa jimbo lake la MBEYA MJINI
Mh. Joseph Mbilinyi akipongezwa na Spika wa Bunge Mh Anne Makinda mara baada ya kula kiapo.
Wednesday, November 10, 2010
SUGU NDANI YA MJENGO ( Kumekucha Bungeni )
Joseph Mbilinyi ngulii wa Bongo Fleva aka MR. II aka Sugu akiwa katika pozi nje ya mjengo wa bunge baadhi ya watu walisema kuwa hataweza lakini mvua ya ushindi wa kura alizopata kutaka kwa wananchi wa jimbo la Mbeya mjini ndizo zilizowakata ngebe wabaya wake kama kina nanihiii
Sugu akiongea na wandishi wa habari katika eneo la Bunge leo , aliwaambia waandishi kuwa kuja bungeni ni kama anakuja kuanza Form I lakini baada ya kuwakuta makamanda wa habari aliofarijika sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)