Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Tuesday, September 13, 2011

MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI AENDELEA NA ZIARA ZAKE KATIKA JIMBO LA MBEYA MJINI NA KUTOA MISAADA


Kabla ya Ziara Mheshimiwa MBUNGE anakutana na Wananchi Ofisini kwake na Kuzungumza nao



  
Ofisini kwa Mh.Mbunge Joseph Mbilinyi akisikiliza shida za Wananchi kabla hajaanza Ziara

                                                                                Mh.Joseph Mbilinyi akipokelewa na Viongozi Mbalimbali wa Kata ya Itende   

Utambulisho na Maelekezo Mbalimbali kabla hajaanza Safari ya Kwenda kuangalia Miradi ya Maendeleo likiwemo Daraja ambalo limekuwa Kikwazo cha Mda mrefu kwenye Kata hiyo

Mh.Sugu akiongozana na Mamia ya Wananchi waliojitokeza kumlaki akielekea Ofisi ya Diwani ili kufanya nae Mazungumzo

Sugu akivuka Daraja ambalo wananchi walimuomba Msaada wa kulitengeneza.,


Mamia ya Wakazi wa Kata ya Itende wakimsindikiza Mbunge wao hadi Ofisi ya Kata

 Nje ya Ofisi ya Kata.., Kuanzia kulia ni Katibu wa Mbunge Mkoloni,

Viongozi mbalimbali wa CHADEMA na wa Kata ya Itende nje ya Ofisi ya Kata ya Itende


Ndani ya Ofisi ya Mtendaji

Diwani wa Kata ya Itende (CCM) akipokea Msaada wa Pesa toka kwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (CHADEMA) ili kukamilisha Ujenzi wa Daraja ambalo limekuwa kikwazo kwa Mda mrefu

Wananchi wakitamani kuingia Ofisini kwa Mtendaji ili kukaa na Mbunge wao

Dirishani nako ni Kundi la Watu

Mazungumzo ya hapa na pale na shukrani

Mamia wakiondoka Ofisi ya Kata na Kumsindikiza Mbunge wao hadi lilipo Daraja., kila mtu alikuwa akiimba vile ajuavyo.!! ila Neno kubwa "Asante Sugu"

Diwani wa Kata ya Itende (CCM) Mh.Weston Kibona akitoa Maelekezo kwa Mbunge wa Mbeya Mjini
 Mh.Sugu akitoa Maagizo kwa Diwani na Wananchi kukamilisha Daraja hilo haraka ili shughuli za Kimaendeleo ziendelee kwani ameshatoa Kiasi cha Pesa kitakacho weza kukamilisha Ujenzi huo
Akipokea Maoni na Maswali na Shukrani kutoka kwa Wananchi


 "Tushikamane ili kuleta Maendeleo"


Mh.Mbunge na Mamia ya Wakazi wa Itende

Na sasa tumsindikize Mbunge wetu

 Akisalimiana na Wazee wa Kata ya Itende

 Kutoka kulia ni Chris Mwamsiku Katibu wa CHADEMA Mbeya Mjini,Mh.Sugu na Diwani wa Itende Weston Kibona

"Asante sana Mh.Mbunge nakutakia Safari njema na Uje Siku ya Ijumaa kukagua kumalika kwa Ujenzi wa Daraja hili Maana umetupa Msaada Mkubwa sana ambao sisi tulikwama"-Weston Kibona Diwani(CCM)

"Waoooh Mbunge wetu., Karibu sana na tumefurahi kukuona.!!"
Mh.Sugu akikagua Majengo amabapo Ofisi za CHADEMA zitajengwa, aliahidi kutoa Mchango katika Ujenzi huo pia
Mazungumzo na Viongozi

Kila Mmoja alikuwa bega kwa bega kwa kila Hatua aliyopita Mbunge
Njiani ni Salam kwa kila Mmoja
Bomba la Maji Masafi la SOGEA SATOM linaloaminika kutatua Matatizo ya Maji Jijini Mbeya likiwa limepita Maeneo ya Itende

 Salam Sugu

Maeneo ya Stand ya Pikipiki (Bodaboda) Mh.Sugu alisimama Kuzungumza na Vijana wa Eneo hilo

Saturday, September 10, 2011

Mh. Joseph Mbilinyi Atoa Pole kwa Watanzania kufuatia kuzama kwa Meli ya Spice huko Zanzibar


Meli ya LCT Spice Islanders ikiwa imezama Pwani ya Nungwi.

Mh. Joseph Mbilinyi ametoa Pole kutokanana na Taarifa za Kuzama kwa Meli ya LCT SPICE ISLANDERS ambayo imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Kwa Taarifa za Awali zinasema kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mh Issa Haji Ussi amethibitisha tukio hilo na kusema ajali  imetokea milango ya saa 8:30 za usiku wa kuamkia leo, na kuongezea kuwa  meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.

Mh Ussi  amesema meli hiyo iliyokuwa imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.

Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Habari hii ni kwa Hisani ya www.wakalinext.blogspot.com

Friday, September 9, 2011

MHESHI MIWA JOSEPH MBILINYI (SUGU) AKIENDELEZA HARAKATI HUKO IGUNGA





Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.
Wananchi wa Igunga wakielekea kwenye mkutano wa CHADEMA.
 


Tuesday, September 6, 2011

MKUTANO WA HADHARA WA MHESHIMIWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI MAENEO YA SIDO MWANJELWA TAREHE 5-9-2011

Mh. sugu akipokelewa na Maelfu ya Wananchi kwa shangwe

Asalaaaaaam..!!!

Mh. Peter Msigwa nae akiwasili


Makamanda wa CHADEMA wanaopigania Haki za Watanzania wakiketi tayari kwa Mkutano

Upande wa Magharibi


Mashariki nako hakukuwa na Njia ya Kupitika

Upande wa Barabarani nako ni Mshikemshike


Viongozi mbalimbali wa Chama na Wananchi wakiwa Wanafuatilia kwa Makini kila kinachoendelea


John Mwambgija maarufu kwa jina la Mzee wa Upako akimkaribisha Ndugu Fred Mpendazoe Kuwasilim Wakazi wa Mbeya..,

Mpendazoe akihutubia wakazi wa Mbeya

"Tutashinda" Kitabu hiki kilinunuliwa sana na Wakazi wa Mbeya.., Ni Kitabu kilichotungwa na Fred Mpendazoe chenye kuelezea Mambo mbalimbali yenye kuifanya Nchi ipate Mwelekeo Mzuri

Fred Mpendazoe Kazini


Mch. Peter Msigwa Mzee wa Weaper akitoa Salam kwa Wananchi wa Mbeya



Wiper zenye Kuashiria Umoja na Mshikamano zikaanza..,  Kuliaaaa


Ni Nomaaa.., Msigwa alitikisa Jiji kwa Style yake ya Wiper kama inavyoonekana.!


Mh. Sugu akipanda Jukwaani tayari kwa Kuzungumza na Maelfu ya Wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini

Mh. Joseph Mbilinyi akisisitiza Jambo

Wananchi wakimshangilia kwa Furaha Mbunge wao ambaye alikuwa akitoa Salam za Bungeni

Sugu Kazini

MASWALI NA MAONI KWA MBUNGE/ SALAM ZA WANANCHI KWA MBUNGE

Kijana Alex Fednand amabaye alikuwa najihusisha na Biashara ya Umachinga akitoa Ushuhuda wa Jinsi alivyokamatwa na Askari na kupotezewa Mali zake

Mzee Yesaya Mwakajile alimuomba Mbunge wa Mbeya Mjini amsaidie kupata Haki ya Mafao baada ya Kustaafu, alikuwa anafanya Kazi Wizara ya Afya

Mwanafunzi wa Sekondari ya Mt. Aggrey alimuomba Mh. Sugu asaide swala kukuza Vipaji Mashuleni ambalo kwa sasa limesahaulika kwa kiwango kikubwa pamoja na Kompyuta.., Mheshimiwa Sugu alisema swala la vipaji mashuleni ni moja ya Sera zake na litatatuliwa huku akimuhakikishia kwa Upande wa Kompyuta kuwa anamalizia Mazungumzo na Kampuni ya SAMSUNG ili kompyuta hizo zije mara moja,
Dada Mwanaharakati kama alivyojitambulisha aligusia Swala la Bank ya Wanawake na NGO'S za Kitapeli zinazoanzishwa Mkoani Mbeya...,Mh. Sugu alimuahidi kuwa kuna Mpango kabambe wa kuanzishwa Community Bank Mkoani Mbeya hivyo itawanufaisha Wananchi wengi wa Mbeya pia Alikemea uwepo huo NGO'S feki kama ilivyolezwa na kuzitaka ziache mara moja

Mama huyu alimulezea Sugu Jinsi Kesi yake iliyodumu kwa zaidi ya Miaka 7 na Jinsi asivyotendewa Haki hivyo anaomba Msaada, Mh. Sugu alimuomba afike Ofisini ili wajue wapi wataanzia kutatua Tatizo hilo

Ndugu A.C Mzee wa Jiji alipanda Jukwaani kwa Niaba ya Wakazi wa Jiji la Mbeya kumpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini kwa Jinsi anvyojituma kuwa karibu na Wananchi ili kujua Changamoto zinazowakabili ingawa ni muda mfupi sana tangu ameingia Madarakani..,

Mh. Sugu akiondoka huku Umati Mkubwa wa Wananchi ukitaka walau kumuona kwa Ukaribu na Kumshika Mkono, palikuwa hapapitiki.!! huyu ndiye Sugu wa Vijana, Wazee,Watoto na kila Mtu.!!

BAADHI YA MAMBO ALIYOYAZUNGUMZIA MH. SUGU KWENYE MKUTANO HUU

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi alizisifu Juhudi za Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bwana. Jumanne Idd ambaye wanashirikiana Pamoja kwa Nia ya kuhakikisha Mbeya inasonga Mbele kimaendeleo

  • Atolea Ufafanuzi juu ya Tv Mbeya ambayo kwa sasa wapo kwenye Mchakato ili ianze kurusha Matangazo yake kwa Nyanda za Juu Kusini

  • Asema ni Lazima kwa kipindi hiki cha Uongozi wake ahakikishe Matatizo ya Maji yanatatuliwa na Barabara ya LAMI kwa Kilomita 29 ni Lazima Ijengwe.
Aelezea Wazo lake la Kuanzishwa kwa Mchezo wa Jackpot Jijini Mbeya lenye nia kukuza Kipato kwa Wananchi na Serikali ili kukwepa Adha ya Kukusanya Michango kwa Wananchi
Awaomba Madiwani ambao wanaamini maeneo yao yanfaa kwa Uchimbaji wa Mabwawa ya Samaki wapeleke Majina ya Kata zao ili Miradi hiyo mianze mara moja
  • Atoa Wazo la kuwepo kwa Kombe la MBUNGE kwenye Michezo mbalimbali ikiwemo Football, pia Nia ya Kuanzaishwa kwa Mapambano mbalimbali ya Ngumi. 
  • Ahidi Ujenzi wa Taa za Barabarani ni Lazima Ukamilike
Ahidi kuendelea kwa Tamasha la Burudani Nyumbani lenye nia kukuza Vipaji na Kuwapa Fursa Wafanya Biashara mbalimbali kuuza Bidhaa zao wakati wote wa Tamasha hilo.