Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Tuesday, September 6, 2011

MKUTANO WA HADHARA WA MHESHIMIWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI MAENEO YA SIDO MWANJELWA TAREHE 5-9-2011

Mh. sugu akipokelewa na Maelfu ya Wananchi kwa shangwe

Asalaaaaaam..!!!

Mh. Peter Msigwa nae akiwasili


Makamanda wa CHADEMA wanaopigania Haki za Watanzania wakiketi tayari kwa Mkutano

Upande wa Magharibi


Mashariki nako hakukuwa na Njia ya Kupitika

Upande wa Barabarani nako ni Mshikemshike


Viongozi mbalimbali wa Chama na Wananchi wakiwa Wanafuatilia kwa Makini kila kinachoendelea


John Mwambgija maarufu kwa jina la Mzee wa Upako akimkaribisha Ndugu Fred Mpendazoe Kuwasilim Wakazi wa Mbeya..,

Mpendazoe akihutubia wakazi wa Mbeya

"Tutashinda" Kitabu hiki kilinunuliwa sana na Wakazi wa Mbeya.., Ni Kitabu kilichotungwa na Fred Mpendazoe chenye kuelezea Mambo mbalimbali yenye kuifanya Nchi ipate Mwelekeo Mzuri

Fred Mpendazoe Kazini


Mch. Peter Msigwa Mzee wa Weaper akitoa Salam kwa Wananchi wa Mbeya



Wiper zenye Kuashiria Umoja na Mshikamano zikaanza..,  Kuliaaaa


Ni Nomaaa.., Msigwa alitikisa Jiji kwa Style yake ya Wiper kama inavyoonekana.!


Mh. Sugu akipanda Jukwaani tayari kwa Kuzungumza na Maelfu ya Wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini

Mh. Joseph Mbilinyi akisisitiza Jambo

Wananchi wakimshangilia kwa Furaha Mbunge wao ambaye alikuwa akitoa Salam za Bungeni

Sugu Kazini

MASWALI NA MAONI KWA MBUNGE/ SALAM ZA WANANCHI KWA MBUNGE

Kijana Alex Fednand amabaye alikuwa najihusisha na Biashara ya Umachinga akitoa Ushuhuda wa Jinsi alivyokamatwa na Askari na kupotezewa Mali zake

Mzee Yesaya Mwakajile alimuomba Mbunge wa Mbeya Mjini amsaidie kupata Haki ya Mafao baada ya Kustaafu, alikuwa anafanya Kazi Wizara ya Afya

Mwanafunzi wa Sekondari ya Mt. Aggrey alimuomba Mh. Sugu asaide swala kukuza Vipaji Mashuleni ambalo kwa sasa limesahaulika kwa kiwango kikubwa pamoja na Kompyuta.., Mheshimiwa Sugu alisema swala la vipaji mashuleni ni moja ya Sera zake na litatatuliwa huku akimuhakikishia kwa Upande wa Kompyuta kuwa anamalizia Mazungumzo na Kampuni ya SAMSUNG ili kompyuta hizo zije mara moja,
Dada Mwanaharakati kama alivyojitambulisha aligusia Swala la Bank ya Wanawake na NGO'S za Kitapeli zinazoanzishwa Mkoani Mbeya...,Mh. Sugu alimuahidi kuwa kuna Mpango kabambe wa kuanzishwa Community Bank Mkoani Mbeya hivyo itawanufaisha Wananchi wengi wa Mbeya pia Alikemea uwepo huo NGO'S feki kama ilivyolezwa na kuzitaka ziache mara moja

Mama huyu alimulezea Sugu Jinsi Kesi yake iliyodumu kwa zaidi ya Miaka 7 na Jinsi asivyotendewa Haki hivyo anaomba Msaada, Mh. Sugu alimuomba afike Ofisini ili wajue wapi wataanzia kutatua Tatizo hilo

Ndugu A.C Mzee wa Jiji alipanda Jukwaani kwa Niaba ya Wakazi wa Jiji la Mbeya kumpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini kwa Jinsi anvyojituma kuwa karibu na Wananchi ili kujua Changamoto zinazowakabili ingawa ni muda mfupi sana tangu ameingia Madarakani..,

Mh. Sugu akiondoka huku Umati Mkubwa wa Wananchi ukitaka walau kumuona kwa Ukaribu na Kumshika Mkono, palikuwa hapapitiki.!! huyu ndiye Sugu wa Vijana, Wazee,Watoto na kila Mtu.!!

BAADHI YA MAMBO ALIYOYAZUNGUMZIA MH. SUGU KWENYE MKUTANO HUU

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi alizisifu Juhudi za Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bwana. Jumanne Idd ambaye wanashirikiana Pamoja kwa Nia ya kuhakikisha Mbeya inasonga Mbele kimaendeleo

  • Atolea Ufafanuzi juu ya Tv Mbeya ambayo kwa sasa wapo kwenye Mchakato ili ianze kurusha Matangazo yake kwa Nyanda za Juu Kusini

  • Asema ni Lazima kwa kipindi hiki cha Uongozi wake ahakikishe Matatizo ya Maji yanatatuliwa na Barabara ya LAMI kwa Kilomita 29 ni Lazima Ijengwe.
Aelezea Wazo lake la Kuanzishwa kwa Mchezo wa Jackpot Jijini Mbeya lenye nia kukuza Kipato kwa Wananchi na Serikali ili kukwepa Adha ya Kukusanya Michango kwa Wananchi
Awaomba Madiwani ambao wanaamini maeneo yao yanfaa kwa Uchimbaji wa Mabwawa ya Samaki wapeleke Majina ya Kata zao ili Miradi hiyo mianze mara moja
  • Atoa Wazo la kuwepo kwa Kombe la MBUNGE kwenye Michezo mbalimbali ikiwemo Football, pia Nia ya Kuanzaishwa kwa Mapambano mbalimbali ya Ngumi. 
  • Ahidi Ujenzi wa Taa za Barabarani ni Lazima Ukamilike
Ahidi kuendelea kwa Tamasha la Burudani Nyumbani lenye nia kukuza Vipaji na Kuwapa Fursa Wafanya Biashara mbalimbali kuuza Bidhaa zao wakati wote wa Tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment