- Msiba ulifanyika Makunguru Mbeya na baadaye maziko kijijini Namba Wani wilayani Rungwe
Saturday, July 26, 2014
Thursday, July 24, 2014
VIONGOZI CCM WATIMULIWA MKUTANONI
Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM, Mkoani
Mbeya, Fatuma Kasenga (aliyekumbwa na dhahama hiyo), akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilayani Rungwe, Mwalimu Peter Gwandege Nkanje.
Wananchi wa Kata ya Kambasegela
wilayani Rungwe mkoani hapa, wamewafukuza viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM
wa kata hiyo walipotaka kufanya mkutano wa hadhara ili kuimarisha chama chao.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika
ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga, Katibu
wa jumuiya hiyo Kata ya Kambasegela, Frank Mwansasu, alisema wananchi
walimtimua yeye na msafara wake kwa madai kwamba waliahidiwa maji zaidi ya
miaka kumi sasa bila kupatiwa.
“Mwenyekiti, kero yangu kubwa ni
kwamba, mimi na wenzangu tulifukuzwa na wananchi tusifanye mkutano wa hadhara
wakati wa ziara yetu ya kata, wananchi wanasema waliahidiwa maji, lakini
hawajapelekewa mpaka hivi sasa,” alisema Mwansasu.
Akijibu kero hiyo, Mwenyekiti
Kasenga, alisema hayo ni matokeo ya baadhi ya viongozi kutowajibika vema katika
nafasi zao.
Alisema suala hilo limemsikitisha,
na kwamba yeye na msafara wake watalifikisha kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Mbeya, Godfrey Zambi, ili kulipatia ufumbuzi.
Akiwa katika ziara hiyo, mwenyekiti
huyo alipokea kero nyingine kwa baadhi ya wananchi wa Kata ya Nkunga, ambao
walimwambia kuwa chama hicho kinachukiwa kwa udhaifu wa baadhi ya viongozi
wake.
Wananchi walisema kata hiyo ina
uhitaji wa umeme, na kwamba katika Kijiji cha Ibililo, kuna msigano wa
viongozi, jambo ambalo linasababisha kutopatikana kwa maendeleo ya kijiji.
“Jitokezeni kwenye marekebisho ya
daftari la kudumu la mpiga kura na ukifika wakati wa uchaguzi, wazee, vijana na
wanawake wanaofaa wapeni nafasi wagombee,” alisema Kasenga.
- Gordon Kalulunga
·
Saturday, July 19, 2014
JOSEPH MBILINYI "SUGU" AITEKA MAFINGA, MUFINDI - IRINGA.
- NI KATIKA MUENDELEZO WA OPERESHENI KOMBOA MUFINDI
- OFISI ZA CHADEMA KATA KUANZA KUJENGWA MUFINDI YOTE
- WILLY MUNGAI “BIG WILLY” AKABIDHI HUNDI NA KUELEZEA MPANGO HUO
- PATRICK OLE SOSOPI NA MWAMBIGIJA “MZEE WA UPAKO" WATOA MISUKULE
William Mungai "Big Willy" akielezea kwa kina jinsi ambavyo program ya kujenga ofisi za CHADEMA katika kata zote za Mufindi Kusini utakavyotekelezwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Mwambigija "Mzee wa Upako" akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiongea na wana Mufindi katika Kikao ambacho kiliambatana na uzinduzi wa Programu ya Ujenzi wa Ofisi za Kata Mufindi.
Makamanda wakiwa wanajadiliana kabla ya kuelekea kwenye Mkutano wa Hadhara
Mh. Joseph Mbilinyi akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Bw. Mwambigija wakiingia eneo la mkutano wa hadhara Mafinga.
Kamanda William Mungai "Big Willy" akifafanua changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa hususani wana Mufindi.
Makamanda wakiwa wamekaa meza kuu huku wakifuatilia mkutano huo wa hadhara.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini Kamanda John Mwambigija almaarufu kama "Mzee wa Upako" akiwa jukwaani kutoa misukule ya CCM.
Joseph Mbilinyi "Rais wa Mbeya" akiwa makini kuangalia umati wa watu uliofurika mara baada ya kupanda jukwaani.
Mbunge wa Mbeya Mjini akiwa jukwaani kuongea na wana Mafinga kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili Tanzania pamoja na mustakabali wa zoezi la Katiba mpya jinsi ambavyo linavyochakachuliwa.
Umati wa wana Mafinga uliofurika ndani na nje ya uwanja wa Mashujaa ukimsikiliza Mbunge huyo.
Wazee wakimpongeza Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya kushuka jukwaani.
Kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge Joseph Mbilinyi Ndg. Kwame Elly Anangisye , Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini John Mwambigija "Mzee wa Upako", Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi " Sugu" na Kamanda Patrick Ole Sosopi wakisimama tayari kwa kuondoka mara baada ya mkutano.
Thursday, July 17, 2014
Wednesday, July 16, 2014
MBUNGE JOSEPH MBILINYI "SUGU" AFANYA ZIARA MTAA WA TONYA - ITUHA, JIMBONI MBEYA MJINI
- APATA FURSA YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUONGEA NA WAKAZI WA ENEO HILO
- VIJANA WALIOCHUKUA KADI ZA CCM SIKU CHACHE ZILIZOPITA WAZISALIMISHA
- WADAI WALIKUWA NA SHIDA NA SHILINGI 5,000 ZILIZOKUWA ZIKIGAWIWA
Vijana wa Mtaa wa Tonya - Ituha walimpokea Mbunge wao kuelekea Tonya
Msafara wa Mbunge kuelekea Mtaa wa Tonya
Mbunge alilakiwa na kikundi cha ngoma cha vijana
Mbunge Joseph Mbilinyi akicheza ngoma baada ya kuwasili mtaa wa Tonya
Msafara wa Mbunge ukaelekea kufungua Ofisi ya CHADEMA -Tonya
Mh. Joseph Mbilinyi akiongea kabla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Tonya ambaye naye ameshiriki katika kuikamilisha
Hapa Mbunge Sugu akijiandaa kuzindua ofisi
Akisaini kitabu cha wageni kuonyesha kuwa ofisi imefunguliwa rasmi
Hapo Mbunge Joseph Mbiliyi akiongea na wakazi wanaoishi kandokando ya daraja hilo
Joseph Mbilinyi "Sugu" hapo akiwa katika mkutano wa hadhara katika Mtaa huo wa Tonya
Wazee nao walikuwepo kusikiliza Mbunge akielezea shuhuli za kimaendeleo zilizofanyika jimboni
Kijana mmojawapo wa aliyechukua kadi ya CCM siku chache zilizopita akinyanyua kadi ya CHADEMA aliyokabidhiwa na Mbunge
Wazee wakimshukuru Mbunge kwa kuwa mwakilishi wao mwema katika jimbo la Mbeya mjini
Vijana wakikabidhiwa kadi za CHADEMA na mbunge wao
Vijana wakiwemo ambao walirudisha kadi za CCM siku chache zilizopita wakiwa wanaonyesha kadi zao za CHADEMA walizokabidhiwa na Mbunge
Wananchi wakionge na Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya mkutano wa hadhara
Baadaye Mbunge Sugu alimalizia na kikao cha ndani na baadhi ya wakazi wa Tonya ambapo pia alipata fursa ya kupokea maoni na maswali na pia alitolea ufafanuzi mambo mbalimbali
Subscribe to:
Posts (Atom)