Wednesday, June 24, 2015
Thursday, June 18, 2015
Monday, June 15, 2015
MBUNGE JOSEPH MBILINYI ALIPOHUDHURIA SHEREHE YA KIMILA YA WASAFWA
- ILIHUSISHA MKUSANYIKO WA
MACHIFU WOTE WA KABILA HILO
- PICHANI CHIFU MKUU
MWANSHINGA AKIMSIKILIZA MBUNGE
MBUNGE JOSEPH O. MBILINYI ANASOMESHA KUPITIA MFUKO WA ELIMU
( muendelezo wa SUGU NA ELIMU - 2 ).....
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O.
Mbilinyi "Sugu" anasomesha wanafunzi katika shule mbalimbali za sekondari, na hii ilitokana na baada ya kuanza kazi ya Ubunge
moja ya changamoto aliyokumbana nayo ni wingi wa walezi na wanafunzi waliofika ofisini au waliomuona kwa ajili ya kuomba msaada wa kusaidiwa ada na
gharama nyingine za shule, ndipo ikapelekea aanzishe Mbeya Education Trust Fund
(METF) au Taasisi ya Mfuko wa Elimu Mbeya.
Ambapo taasisi hii METF katika moja ya jukumu lake imeweza
kusaidia wanafunzi wa sekondari
takribani 270 waliofaulu na hawakuwa na uwezo kutokana na kuwa wanatoka kwenye familia zenye uwezo
mdogo kiuchumi kwa kuwalipia ada na sare za shule pamoja na
mahitaji mengine ya elimu pale inapobidi, na ilipoanza mwaka 2013 ilianza na watoto wa kidato cha 1 mpaka 4 (o'level) lakini sasa imeweza kusaidia mpaka wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 (A level).
(Chini ni picha mbalimbali za baadhi ya watoto wanaosomeshwa na Mfuko huu wakiwa na Afisa wa METF)
Sunday, June 14, 2015
MBUNGE "SUGU" AIBUKIA KISIWANI MAFIA
• AFANIKIWA KUTOA VIONGOZI WA CHADEMA POLISI
• ATEMBELEA VIJIWE NA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA
Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA Joseph O. Mbilinyi "Sugu" wikiendi hii alikuwa kwenye ziara ya ujenzi wa Chama kwenye kisiwa cha Mafia na kufanikiwa kufanya mambo kadha wa kadha ya ujenzi wa Chama.
Katika ziara yake hiyo ambayo licha ya kutembelea vijiwe mbalimbali na kubadilishana mawazo na wakazi wa kisiwa hicho pia alikumbana na mkasawa kushikiliwa kwa viongozi wa CHADEMA kisiwani hapo kwa makosa yasioeleweka ambapo kikosi hicho cha Mbunge huyo wa Mbeya waliweza kupigania mpaka usiku wa manane kuhakikisha viongozi hao wanatolewa polisi.
Pia katika ziara hiyo Mbunge pia aliweza kuongea na viongozi wa Kata katika jimbo hilo la Mafia pamoja na kusalimiana na vijana wa kikosi cha Red Brigade katika kisiwa hicho pamoja na kusaini kadi nyingi za CHADEMA ambazo wakazi wa kisiwa hicho walikuwa wakizihitaji kwa udi na uvumba.
Baadaye jumapili aliweza kuongea na wakazi wa kisiwa hicho kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani hapo na kusisitiza elimu ya uraia ikiwemo kutoogopa vitisho vya polisi ambao ni vibaraka wa chama tawala.
Mbunge huyo pia alivutiwa na mandhari tulivu ya kisiwa hicho na huku akiwa amefikia katika chumba ambacho akina AC wala TV ambapo kwa madai yake alisema ni kizuri kwa utulivu na kutafakari.
KUTOKA OFISI YA MBUNGE MBEYA MJINI..... (SUGU NA ELIMU - 1)
IJUE PROGRAMU YA KOMPYUTA
MASHULENI
Mbunge
wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi anaendesha programu ya mafunzo ya kompyuta
kwa wanafunzi wa sekondari za Kata zilizopo jijini Mbeya ambapo tayari
ameanzisha madarasa ya kompyuta katika shule za sekondari tano (5) kati ya 10 ambazo zitafikiwa na mradi huu
kwa awamu ya kwanza, shule hizo ni Shule
ya Sekondari Mwakibete, Shule ya Sekondari Uyole, Shule ya Sekondari Forest,
Shule ya Sekondari Iwambi na Shule ya Sekondari Iganzo.
Lengo la programu hii ni kuhakikisha wanafunzi wa shule za Mbeya wanapomaliza kidato cha nne (4) wawe na uwezo wa kutumia kompyuta hali iliyopelekea kuongeza
hadhi za shule na elimu kwa ujumla katika shule za Kata jijini Mbeya
Monday, August 11, 2014
Friday, August 8, 2014
SUGU AWALAUMU POLISI KURUSHA MABOMU MBEYA
Mbunge wa Mbeya mjini,
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amelishutumu Jeshi la Polisi mkoani humo kuwa ndiyo
chanzo cha vurugu baada ya juzi kutumia mabomu ya machozi kuwazuia wafuasi wa
Chadema na waombolezaji kuubeba mikononi mwili wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
wa Itiji, Ezekiel King kwa lengo la kutembea nao kwa miguu kutoka
Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi nyumbani kwake Itiji kuuzika.
Baada ya mabomu hayo
kurushwa, viongozi na waombolezaji walilazimika kulibwaga chini jeneza la mwili
wa marehemu na kuanza kukimbia.
Marehemu alifariki dunia
katika hospitali hiyo, alikopelekwa kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua
ghafla katika Gereza la Ruanda alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka saba
baada ya kupatikana na kosa la kudhuru mwili wa mwanachama wa CCM .
Akizungumzia tukio hilo,
Sugu alisema kilichotokea juzi ni uthibitisho kwamba polisi ndiyo wamekuwa
chanzo cha vurugu.
“Sisi tulikuwa kwenye
msafara wakaja kutuzuia na kuninyooshea bunduki. Tukawaeleza tunakwenda kuzika,
wao wanasema tulitakiwa kuomba kibali cha kwenda kuzika,” alisema Sugu na
kuongeza: “Watu walikuwa wengi na magari ya kuwabeba kwenda kuzika hayakuwepo,
tuliamua kutembea sasa kibali cha nini,” alisema Sugu.
Sugu alisema polisi
wasipobadilika mara moja, wananchi watachukua hatua kuwaondoa katika nyumba
walizopanga uraiani ili wakaishi kituo kikuu cha polisi mkoani humo kwa vile
hawaijali jamii inayowazunguka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed
Msangi aliwataka Chadema kuacha kuwazushia polisi na kuongeza kuwa madai ya
Sugu hayana ukweli wowote.
- Mwandishi Wetu, Mwananchi
Thursday, August 7, 2014
MBUNGE JOSEPH MBILINYI AKABIDHI VIFAA VYA CHAMA KWA BAVICHA JIJINI MBEYA
- KATIBU WA MBUNGE KWAME ELLY ANANGISYE AMKABIDHI MWENYEKITI BAVICHA MBEYA MJINI MOSES MWAIFUNGA KWA NIABA YA MBUNGE
POLISI MBEYA WAFYATUA MABOMU NA KUPORA JENEZA MBELE YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI "SUGU"
- NI LA MAREHEMU KING ALIYEKUWA MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA ITIJI
- ALIFIA GEREZANI ALIKOKUWA ANATUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 7
- RUFAA YA KESI YAKE YENYE UTATA ILIKUWA ISIKILIZWE TAR. 11/8/2014
Subscribe to:
Posts (Atom)