Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Wednesday, September 25, 2013

TANGAZO: MIKUTANO YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI




TASWIRA: MBUNGE JOSEPH MBILINYI AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI MBEYA

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi amekabidhi mchango wake wa cement kwa viongozi wa makanisa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa makanisa ya mbeya mjini yakiwemo Kanisa la Mitume- Mwanjelwa, Kanisa la Moravian-Iyunga na Kanisa Katoliki - Uyole...kama ilivyo ada yake ya  kushiriki katika ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimbo la Mbeya Mjini.
 



Monday, September 23, 2013

SIKU MBUNGE JOSEPH MBILINYI ALIPOONGEA NA WANANCHI WA KYELA

Mh. Joseph Mbilinyi akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Kyela Mbeya
 

Wananchi wa Kyela wakimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini......


Saturday, September 21, 2013

Dr Slaa Awasili Washington DC, Marekani
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipungia mkono baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Dulles nchini Mareani leo tarehe 21 Septemba 2013. Dr Slaa anatarajia kufanya mkutano na Wakazi wa Washington dc tarehe 22 septemba 2013 katika Ukumbi wa Mirage uliopo University BLVD.

Pichani ni makamanda waliojitokeza Uwanja wa Ndege wa Dulles Kumpokea Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ambaye anatarajia kufanya Mkutano na Watanzania wanaoishi Washington DC na maeneo mengine yaliyo karibu.


 

Dr Slaa akipeana Mkono na Katibu wa Tawi na Afisa wa Habari wa Tawi la Chadema Washington DC (DMV) Mh Liberatus Mwang'ombe mara baada ya Dr Slaa kufika Marekani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipeana mkono na Katibu wa Baraza la wanawake Bi Baybe Mgaza uwanja wa ndege wa Dulles alipowasili akitokea Tanzania.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Akipena mkono na Katibu wa Baraza la wazee Mh Elias Mshana uwanja wa ndege wa Dulles Marekani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipeana mkono na Mweka Hazina wa Tawi la Chadema Washington DC (DMV) Mh Ludigo Mhagama kwenye uwanja wa Ndege wa Dulles nchini Marekani.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Akiwa na watoto wa Mbunge wa Viti maalum wa Chadema Kwimba Mh Leticia Nyerere, Julia Nyerere (Kushoto) na Helena Nyerere (Kulia).

PICHA: MBEYA CITY FC YAITULIZA SIMBA KWA SARE YA MAGOLI 2-2







 KIPINDI CHA PILI KIKIWA KINAENDELEA
 MASHABIKI WAKIWA WANAFUATILIA MECHI KWA UKARIBU 


 MBEYA CITY WAKIWA WAMEPATA GOLI LA PILI
 MBEYA CITY FC WAKISHANGILIA GOLI LAO LA PILI

 MASHABIKI WA MBEYA CITY FC WAKIWA WANASHANGILIA GOLI LA PILI

KOCHA MKUU WA MBEYA CITY FC BWANA MWAMBUSI WA KWANZA KUTOKA KUSHOTO AKIFUATILIA MECHI KWA UMAKINI.
 MASHABIKI WA SIMBA WAKIWA WAMEPOA BAADA YA M BEYA CITY FC KURUDISHA GOLI
 MASHABIKI WA MBEYA CITY FC WAKIWA WENYE FURAHA 

HAPA ILIKUWA NI PATA SHIKA NGUO KUCHANIKA BAADA YA SHABIKI WA SIMBA KUINGIA ENEO LA MASHABIKI WA YANGA.
 MPIRA UMEKWISHA
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKIWA WANATOKA NJE YA UWANJA BAADA YA MPIRA KWISHA
 WACHEZAJI WA MBEYA CITY FC WAKIWA WANATOKA UWANJANI BAADA YA MPIRA KWISHA

 MASHABIKI WALIO TOKA MBEYA KUSHANGILIA MBEYA CITY FC WAKIWA NJE YA UWANJA WAKIENDELEA KUSHANGILIA MPIRA.

CHANZO: PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

Friday, September 20, 2013

SUGU AWAAGA MASHABIKI WA MBEYA CITY....

  •  Ni baada ya Kukamilisha Ahadi ya Kugharamia baadhi ya gharama ikiwemo Usafiri na Viingilio
  • Inakwenda kucheza na Simba Sports Club...Jumamosi jijini Dar es salaam
      Ni Shangwe Mbunge wa Mbeya Mjini alipokutana na washabiki Mbeya City ili kuwaaga..
  Mh. Joseph Mbilinyi akibadilishana mawazo na Wana Mbeya wanaoelekea kwenye mtiti Dar...
 
  Joseph Mbilinyi  almaarufu kwa jina " Rais wa Mbeya" akiwapa mawaidha mashabiki kabla ya safari yao ya kwenda kuishangilia Mbeya City, Dar es salaam
 
 Tayari wapenzi wa Mbeya City wanachanja mbuga hapo ni mpaka wa Mbeya na Iringa...

Thursday, September 19, 2013

SUGU APIGA TAFU MASHABIKI MBEYA CITY....AMERIPOTI BIG SHAH KWENYE FACEBOOK....

Mheshimiwa Sugu ametoa 1.5 milion na Kiingilio kwa watu 50,
Kuchangia mashabiki wa Mbeya City watakaoenda
Kushuhudia Tukiwafunga Simba pale Taifa siku ya Jumamosi.
Mashabiki mnaopenda kwenda Muone Raysa 714786087.
Mbeya City Stand Up!

Kutoka kwenye facebook,.... wall ya Big Shah

Mheshimiwa Sugu atukabidhi Fedha,
Kwa ajili ya Safari ya Kesho kwenda kushuhudia tukiwafunga Simba
Hapo Jumamosi uwanja wa Taifa.
Mbeya City FC ndio timu Bora msimu huu wa Ligi Kuu.





Taarifa ya Msajili kuhusu raia wa kigeni kushiriki shughuli za kisiasa nchini

19/09/20
PicturePicture

Kosa la Ndugai

Na Edson Kamukara

Naibu Spika akishughulika na simu ya mkononi wakati wa kuongoza Bunge
 


HUKU akijitapa kuwa ndiye mlinzi wa kanuni za Bunge, na akiwalaumu wabunge, hasa wa upinzani, kwa kukiuka kanuni hizo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amebainika kuwa alivunja kanuni nyingi za Bunge siku ilipozuka zogo bungeni.
Kwanza, alivunja kanuni inayomtaka ampe fursa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuzungumza.
Pili, alivunja kanuni inayomruhusu kumchukulia hatua mbunge aliyedharau kiti cha spika.
Tatu, alivunja kanuni inayomtaka kuahirisha Bunge kabla ya kuruhusu askari kuingia bungeni unapotokea mzozo.
Kanuni ya 5 (1) inasema: “Katika kutekeleza majukumu yake yaliyotajwa katika ibara ya 84 ya katiba, spika ataongozwa na kanuni hizi na pale ambapo kanuni hazikutoa mwongozo basi spika atafanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria nyingine za nchi kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya maspika wa mabunge pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa Bunge la Tanzania.” Mbowe hakupewa fursa hiyo.
Kwa utamaduni wa mabunge ya Jumuiya ya Madola ambao unatumiwa na Bunge letu, Mbowe ni sawa na Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Tofauti yao ni moja tu, kwamba waziri mkuu ana dola, na yeye hana.
Kwa kuzingatia utamaduni huo, viongozi hawa wanaposimama wakati wowote, kiti cha spika kitamwomba mbunge anayezungumza aketi chini kisha mmoja kati yao ambaye atakuwa alisimama atapewa nafasi ya kutoa hoja yake.
Kanuni ya 74 - (1) ndiyo ilipaswa kutumiwa na Ndugai kumshughulikia Mbowe kama alidharau kiti, lakini pia hakuitumia.
Inasomeka: “Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikiwa: (a) kwa maneno au vitendo, mbunge huyo anaonyesha dharau kwa mamlaka ya spika; au (b) mbunge huyo anafanya kitendo chochote cha makusudi cha kudharau shughuli ya Bunge au mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.
Kama Ndugai angezingatia kanuni za kudumu zinazoliongoza Bunge ili kudhibiti fujo kama hizo bungeni, alitakiwa kutumia kanuni ya 76 - (1) badala ya kuwaingiza ukumbini watu wasiopaswa ili kuwadhalilisha baadhi ya wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wao, Mbowe.
Kanuni hiyo inasema: “Kwa madhumuni ya kudhibiti fujo endapo ikitokea ndani ya ukumbi wa Bunge na spika ataona kuna haja ya kutumia nguvu, basi anaweza kuahirisha shughuli za Bunge bila ya hoja yoyote kutolewa au kusitisha kikao kwa muda atakaoutaja ili fujo hiyo iweze kudhibitiwa na mpambe wa Bunge.”
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanautafsiri uamuzi wa Ndugai kama mbinu ovu iliyokuwa imeandaliwa mapema ili kuwasonga wapinzani wasiweze kuujadili muswada wa sheria wa kurekebisha sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013.
Ni wazi kuwa kasoro nyingi zilizopenyezwa katika muswada huo zisingeweza kuafikiwa na wapinzani ili kuipa nafasi CCM kudhibiti mchakato wa katiba mpya unaoendelea.
Katika vuta ni kuvute hiyo, wapinzani waliitaka serikali kuuondoa muswada huo kisha kuufanyia marekebisho, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau wakiwemo Wazanzibari.
Serikali na kiti cha spika hawakuwa tayari kutekeleza masharti hayo, hatua iliyoibua mvutano wa kikanuni hadi kufikia wabunge kupiga kura ya kuamua ama mjadala uendelee au usitishwe.
Kura za wabunge waliotaka mjadala huo uendelee zilikuwa nyingi kutokana na CCM kuwa na wabunge wengi. Lakini baada ya uamuzi huo, Mbowe alisimama kuomba ufafanuzi wa kikanuni, akakataliwa.
Licha ya Ndugai kumdhalilisha Mbowe, hakufahamu alitaka kusema nini, hatua iliyoibua hamaki kwa wapinzani.
Mbowe alitaka kuomba kiti kiwatake viongozi wa serikali, Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi waweke mezani ushahidi wa vielelezo vya taarifa walizokuwa wamezitoa.
Kwa mujibu wa Mbowe, taarifa hizo hazikuwa na uthibitisho wa vielelezo, na kwamba vile vile zilikuwa na upotoshwaji mwingi, lakini Ndugai hakumpa nafasi hiyo, badala yake alimtaka aketi chini.
Kiongozi huyo, hakuketi bali alisisitiza kuwa ana hoja asikilizwe, jambo lililomfanya Ndugai kuwaita askari ili wamtoe nje bila kujali kama wengine hawapaswi kuingia ukumbini wakati Bunge linaendelea kwa mujibu wa kanuni.
Baada ya askari hao kuitwa na kuingia ndani, wabunge wa upinzani ukimwondoa Augustino Mrema wa TLP (Vunjo), walimzunguka Mbowe wakipinga asitoke nje kwa kuzingatia kuwa Ndugai alikuwa amekiuka kanuni.

SUGU AZIDI KUTAMBA PANDE ZOTE ZA MKOA WA MBEYA: KIWIRA - TUKUYU YASIMAMA KWA MUDA

Hapo Mbunge wa Mbeya Mjini akiongea na wananchi wa Kiwira, kitongoji almaarufu kwa jina la "zote mia"
 
 Umati wa wakazi wa Kiwira wakimsikiliza Mh. Joseph Mbilinyi